• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
KWA KIFUPI: Janga la corona limetatiza pakubwa vita dhidi ya TB nchini

KWA KIFUPI: Janga la corona limetatiza pakubwa vita dhidi ya TB nchini

Na LEONARD ONYANGO

HUKU ulimwengu ukiadhimisha siku ya Kifua Kikuu (TB) Jumatano, imebainikika kuwa janga la virusi vya corona limetatiza juhudi za kupambana na maradhi haya humu nchini.

Ripoti ya vuguvugu la kimataifa la Stop TB Campaign, inaonyesha kuwa janga hili lilisababisha asilimia 20 ya waathiriwa wa TB kukosa vipimo na matibabu kote duniani.

Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa maambukizi ya maradhi haya humu nchini yalikuwa yamepungua kwa asilimia 8.5 kati ya 2019 na 2020 kabla ya janga hili.

Bw Samwel Misoi, Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Kifua Kikuu, Ukoma na Maradhi ya Mapafu, anasema maambukizi ya TB yalipungua katika kaunti 41 kati ya 47 ndani ya kipindi hicho.

Idadi ndogo zaidi ya maambukizi ilishuhudiwa katika Kaunti za Kisumu, Makueni, Lamu na Pokot, kulingana na Bw Misoi.

You can share this post!

PATA USHAURI WA DKT FLO: Vidonda vya mafua huletwa na nini?

Ingwe yapata pigo kusaini wachezaji baada ya FIFA kuipiga...