• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
LISHE: Chagua chakula cha kuzuia matatizo ya kiafya

LISHE: Chagua chakula cha kuzuia matatizo ya kiafya

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WATU wengi hula chakula kikuu na vya bei nafuu ndani ya kila mlo.

Chakula hicho kikuu huwapatia nguvu ya kutosha kuwawezesha kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Lakini chakula hicho kikuu pekee hakitoshi kumfanya mtu awe mwenye afya. Kuweza kukua, kuwa na nguvu, na kupambana na maambukizi, lazima tule vyakula vingine-zaidi ya chakula kikuu.

Tunahitaji nafaka kwa wingi au mimea au mbogamboga zenye wanga kama vile karoti, viazi vitamu, viazi mviringo, maharagwe, kunde za kijani, maboga, magimbi, au matunda.

Kwa kula vyakula tofauti vyenye virutubisho tofauti kila siku, tunaweza kuzuia matatizo makubwa ya kiafya.

Vyakula vyenye wanga hutupatia nguvu

Chakula chetu kikuu chenye wanga huipatia miili yetu kiasi kikubwa cha nguvu ambayo tunahitaji kufanya kazi, na kujihudumia sisi wenyewe pamoja na familia zetu. Kutegemea mahali unapoishi, chakula kikuu kinaweza kuwa; wali, mkate, mahindi, ndizi, ngano, viazi au mihogo.

Vyakula hivi vyenye wanga vinaweza kupikwa kama uji, kukandwa na kutengeneza mikate na vitafunwa vingine, kupondwa au kusagwa na kutengeneza chakula laini, au kupikwa moja kwa moja.

Chagua nafaka za asili

Kama una fursa ya kuchagua wanga gani utakula, nafaka za asili hustawi kwa urahisi zaidi bila kuhitaji mbolea zenye gharama kubwa, na zina virutubisho vingi zaidi. Mahindi, ngano, na mchele ni nafaka bora. Lakini nafaka za asili kama vile mtama na baadhi ya ngano, ni bora zaidi kwa sababu zina protini, vitamini, na madini zaidi.

Mkate na tambi zilizotengenezewa viwandani kwa kiasi fulani si nzuri

Mkate uliofungashwa, biskuti na tambi hukosa sehemu muhimu ya lishe hitajika ukilinganisha na faida zinazopatikana katika vyakula vikuu vya kawaida ambavyo hupikwa nyumbani kama vile uji na nafaka. Na mara nyingi huwa na kiwango kikubwa cha mafuta, chumvi, na sukari kupita kiasi.

Sukari na mafuta

Sukari na mafuta ni vyanzo vya nishati mwilini, na kiwango kidogo cha vyakula hivi kinahitajika kwa ajili ya afya. Hakikisha watoto wanapata mafuta kidogo katika kila mlo wao hasa kama chakula chao cha kawaida ni wanga zaidi.

Kawaida, vyakula ambavyo vimetengenezewa viwandani huwa na kiwango kikubwa cha mafuta na sukari kuliko kinachohitajika mwilini. Watu ambao hutegemea sana vyakula hivyo hula kaisi kikubwa mno cha sukari na mafuta, hali ambayo huwasababishia matatizo mengi ya kiafya.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Serikali iirai Fifa iondoe marufuku wakati...

Misri wamtimua kocha Ehab Galal baada ya kusimamia mechi...

T L