• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
LISHE: Chagua chakula chenye manufaa kwa mtoto

LISHE: Chagua chakula chenye manufaa kwa mtoto

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MTOTO ana utumbo mdogo hivyo hali sana na ni muhimu kuwa na uhakika kuwa chakula anachokula kinastahili.

Muda mzuri wa kula

Kiujumla, watoto wanaweza kula chakula kuanzia miezi sita na kuendelea. Punde kinapoandaliwa, zingatia ulaji wa mtoto wako.

Lakini pia ni vizuri uzungumze na mkunga au daktari wa watoto kabla ya kumpa mayai, samaki, chungwa, na maziwa ya mtindi kama mtoto wako mdogo ni wa umri chini ya mwaka kwa sababu vyakula hivyo huweza kusababisha mzio.

Vyakula vingine kama nyama, matunda, na mboga mboga ni sahihi wewe mzazi kuanza kumlisha mtoto wa umri wa miezi sita.

Ijapokuwa watoto hukua kwa utofauti, ni vizuri kutafuta ushauri wa daktari au watu wazima ili kujihakikishia punde unapotaka kumuanzishia chakula mtoto na pia kipi ni bora zaidi kwa huyo mtoto wako.

Ndizi

Ndizi zina wanga kumpa mtoto nguvu. Vile vile nyuzinyuzi kwenye ndizi zinasaidia mmeng’enyo wa chakula.

Ndizi ni chakula kizuri na chepesi kwa mtoto, na huwa rahisi kuiva.

Pindi unapoandaa ndizi kwa mtoto mdogo, hakikisha imeiva vizuri na imepondeka vizuri.

Kwa mtoto mkubwa, anaweza kula ndizi kama ilivyo yaani nzima. Lakini iwe pia imeiva vizuri ili iwe rahisi kwa mtoto kuisaga na kuimeza kwa urahisi zaidi.

Viazi vitamu

Viazi vitamu huwa na potassium, vitamini C, na nyuzinyuzi kwa wingi. Pia husaidia kulinda watoto dhidi ya magonjwa.

Watoto wengi hupenda viazi vitamu zaidi kwasababu ya ladha yake ya utamu wa asili.

Viazi. PICHA | MARGARET MAINA

Punde unapopika hivi viazi, viponde au kusaga. Viazi vitamu vina ulaini ambao ni rahisi kwa mtoto kuvila, hata kwa watoto ambao ndo wanaanzishiwa kula vyakula vigumu.

Parachichi

Parachichi huwa na protini nyingi katika mafungu ya matunda na huwa na mafuta mazuri.

Aina hii ya mafuta hulinda moyo.

Hakikisha unampa mtoto parachichi liloiva vizuri. Osha nje ya hilo tunda kisha menya maganda na lisage liwe laini.

Sababu lina mafuta mengi, mtoto hushiba mara baada ya kula. Mpe kidogo na chakula kingine kama kuku au nyama laini.

Mayai

Mayai ni mazuri kwa kuwa yana protini na huwa na vitamini kadhaa. Wakati mayai ni chanzo kikuu cha protini. Pata ushauri wa mtaalam wako wakati mtoto wako ameanza kula vyakula kuangalia kama ni sawa au wakati gani itakuwa sawa kumpa mayai mtoto wako.

Mayai mazuri ni ya kienyeji na sio ya kuku wa kisasa.

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Kiswahili ni mhimili mkuu wa kuhifadhi...

Didmus Barasa asema anayefaa kukamatwa ni Raila

T L