• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
LISHE: Umuhimu wa tunda la kantalupu

LISHE: Umuhimu wa tunda la kantalupu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Kantalupu ni aina ya tikiti ambalo ni tamu sana, ingawa lina sura isiyo ya kawaida.

Limejaa virutubisho vingi.

Kama matunda na mboga nyingi, kantalupu pia lina maji ya kutosha. Uoevu hufanya kantalupu kuyeyuka polepole mwilini mwako na hivyo ulaji wa kantalupu hautafanya sukari yako ya damu kuongezeka. Kwa hivyo tunda hili ni chaguo bora kwa watu wenye ugonjwa wa sukari.

Kantalupu. PICHA | MARGARET MAINA

Kantalupu huwa na Vitamini C na uwezo wake pia uko kwa kuzuia seli zako kutokana na uharibifu.

Linasaidia mlaji kupata Vitamini A, ambayo husaidia kuweka macho yako katika ubora unaofaa. Si hayo tu kwani nayo ngozi, mifupa, na mfumo wa kinga huimarika kabisa.

Potasiamu inayopendekezwa kila siku, muhimu kwa moyo wako, misuli na kukabili tatizo la shinikizo la damu.

Unyevu

Kantalupu huwa na vioevu almaarufu kama elektroliti vyenye madini yenye uwezo wa kusawazisha maji ya mwili katika mwili wako. Hiyo hukusaidia kukaa na maji na nishati.

Kusaidia kupambana na magonjwa

Kantalupu ni sehemu nzuri ya lishe yenye afya.

Vitamini C

Kantalupu huwa na kiwango kizuri cha vitamini C ambayo inahusika katika utengenezaji wa mishipa ya damu, gegedu, misuli, na kolageni katika mifupa.

Folati

Maneno folati yaani folate na asidi ya Folic hutumia kurejelea Vitamini B-9. Ingawa hivyo folati ni neno linalotumiwa kurejelea vyakula vyenye Vitamini B-9 asili ilhali asidi ya Folic ni neno linalotumiwa kwa virutubisho na vyakula vilivyoimarishwa. Folate inajulikana sana kwa kuzuia kasoro za kuzaliwa kama vile bifida ya uti wa mgongo.

Nyuzinyuzi

Kantalupu huwa na nyuzinyuzi zilizo muhimu kwa afya na zenye uwezo mkubwa kuzuia kuvimbiwa. Lishe yenye nyuzi nyingi inaweza:

–         kupunguza hatari yako ya ugonjwa wa moyo na kisukari

–         kukusaidia kupunguza uzito kwa kukufanya ujisikie kamili kwa muda mrefu

Shinikizo la damu

Nyuzinyuzi, potasiamu, vitamini C, na choline katika tikitimaji vyote vinasaidia afya ya moyo.Kula vyakula vyenye potasiamu nyingi kunaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu.

Ngozi na nywele

Vitamini A huchangia ukuaji na udumishaji wa tishu zote mwilini, zikiwemo zile za ngozi na nywele.

Vitamini C huwezesha mwili kutoa kolageni, ambayo hutoa muundo wa seli, ngozi na nywele.Anuwai ya madini na vitamini inaweza kuchukua jukumu katika kukuza ukuaji wa nywele na kuzuia upotezaji wa nywele.

  • Tags

You can share this post!

TANZIA: ‘Ker’ wa Waluo afariki

Zifahamu baadhi ya faida za upupu (stinging nettle)

T L