• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
FASIHI SIMULIZI: Tathmini ya kipera cha Miviga katika utanzu wa Maigizo

FASIHI SIMULIZI: Tathmini ya kipera cha Miviga katika utanzu wa Maigizo

Na KIPKOROS BORWO

ALHAMISI hii, tunaendelea kuangazia kitanzu cha miviga.

Tutataja tu, japo kwa akali aina zaidi za miviga, umuhimu wake na changamoto zake kwa jamii.

Aina nyingine za miviga:

i) Sherehe za kuzaliwa kwa watoto, kwa mfano, kuzaliwa Yesu (Krismasi kwa waumini Wakristo) iliyofurahiwa 25/12/21

ii) Sherehe za kuwapa watoto majina

iii) Kuapishwa kwa viongozi

iv) mahafala ya kuhitimu chuoni/askari

v) kupeleka na kupokea posa

vi) malumbano ya kuafikiana mali za ndoa

vii) sherehe za baada ya mavuno mazuri

viii) ushindi wa kivita na askari

ix) sherehe za kuadhimisha Sikukuu za kitaifa au majagina katika jamii.

Umuhimu wa miviga katika jamii

i) Umoja na ushirikiano; Miviga hukuza umoja na ushirikiano baina ya wanjami

ii) Huelimisha; miviga huelimisha wanajamii hasa kuhusu utamaduni wa kila jamiii

iii) Hukuza lugha ya Kiswahili na za kwanza

iv) Utamaduni; huendeleza tamaduni na mila za kila jamii kwa kupitishia kutoka kizazi kimoja hadi kingine

v) Huburudisha; wanajamii kwa kuwapumzisha na kufurahia, kwa mfano, vichekesho na michezo

vi) Huliwaza; miviga huliwaza wanajamii hasa waliofiwa

vii) Historia; huhifadhi historia ya jamii kwa manufaa ya vizazi vijavyo

viii) Ujasiri; hukuza ujasiri wa fanana/waigizaji jukwaani

ix) Vipawa; hukuza na kunoa vipawa vya wanajamii

x) Riziki/pato; huwapa waigizaji na fanani riziki na kuimarisha uvumi

xi) Kitambulisho cha jamii kwani kila jamii ina miviga yake tofauti na nyingine.

Changamoto

i) Maafa/vifo; vijana wanaopashwa tohara wanaweza kuvuja damu hadi kufa.

ii) Ukiukaji wa haki; si haki kwa wasichana/wanawake kupashwa tohara

iii) Magonjwa; kutahiri kwa kutumia wembe mmoja husababisha ukimwona au mkusantiko wa watu shereheni husambaza Uviko-19

iv) Hutia hofu; maapizo huhusu kuwalaani watu na tohara hutia wanajamii hofu tele.

v) Hugharimu pesa nyingi; arusi au mazishi huhitaji pesa nyingi ili kutumia vizuri

vi) Uharibifu wa mazingira; sherehe hizi nyingi huhitaji matawi ya miti mahususi. Aidha husababisha kelele nyingi kama nyimbo na Denis za usiku

vii) Hukinzana na baadhi ya imani za kidini kwa mfano maombi ya kumlaani mtu

viii) Huendeleza ushirikina; jamii nyingi huamini kuwa miungu ndiyo hutekeleza mauaji ya watu waovu katika jamii

ix) Ubadhirifu wa mali; baadhi ya jamii huribu mimea shambani siku ya mazishi ili kuwafukuza mapepo.

x) Siri kali; miviga kama jando inasheheni siri kali ajabu na kutoeleweka kwa jamii Nyingine.(Maneno 291)

Borwo Kipkoros

Shule ya Upili ya Wasichana ya Alliance

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Sokomoko bungeni ni dalili hatari uchaguzini

Kampeni za amani zitaokoa utalii, wadau wasema

T L