• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
CHAKULA CHA UBONGO: Uchangamfu ni kiambata muhimu katika kuyaafiki matilaba yako

CHAKULA CHA UBONGO: Uchangamfu ni kiambata muhimu katika kuyaafiki matilaba yako

Na HENRY MOKUA

JE kukosa utulivu, kuwa na fikra hasi kuna athari gani?

Kwa mujibu wa muuguzi Richard J. Davidson, pana tofauti kubwa baina ya bongo za watu wenye mihemko chanya (positive emotions) na wenye bongo zinazosheheni mihemko hasi (negative emotions).

Mtafiti wa Saikolojia Kalin akishadidia utafiti huu anasema: Wanasayansi wameanza kuondoa makini yao kwenye matatizo yanayosababisha magonjwa na kuyaelekeza kwenye hali za bongo zinazozuia fikra chanya na uhusiano wayo na hali za kisaikolojia kama mambo yanayoathiri afya.

Wanachosema wanasayansi hawa ni kwamba fikra safi, fikra chanya huchangia pakubwa katika akili kuyashika anayofunzwa au kuyasoma mtu kuliko mwenye fikra kadha wa kadha kuhusiana na kutobahatika kwake.

Maradhi yanayowapata wanafunzi wakati mwingine yasingewapata endapo wangejifunza umuhimu wa uchangamfu, ushirikiano na fikra chanya. Lakini kwa kushinda wakijihurumia, wanajipunguzia kinga ya mwili dhidi ya magonjwa pasi na kujua.

Ili kudhibiti hali hii ewe mwanafunzi kumbuka kuwaza kupindukia na kujihurumia hakuwezi kubadili kitu.

Badala yake jiaminishe kwamba hakuna kilicho aushi duniani, cha pekee kinachodumu ni mabadiliko.

Jihakikishie kwamba hali yako ya sasa si ya kudumu bali ya kupita tu.

Kwa msingi huu, ibuka na mikakati ya kuhakikisha kwamba katikati ya kipindi kifupi utaibatilisha hali inayoikumba familia yako.

  • Tags

You can share this post!

Mbinu za mrengo wa ‘Tangatanga’ kuchelewesha...

Mbinu za Ukulima: Teknolojia ya trei kukuza miche

T L