• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Makahaba wakongwe waapa kukatalia mijini wakidai wanatafutia wajukuu maisha mazuri

Makahaba wakongwe waapa kukatalia mijini wakidai wanatafutia wajukuu maisha mazuri

NA RICHARD MAOSI

MAKAHABA wakongwe wameapa kuendelea kukatalia mijini wakidai wanatafutia wajukuu wao maisha mazuri kabla ya kustaafu.

Taifa Leo Dijitali imebaini kuwa wengi wao wameshindwa kabisa kuachana na biashara ya ngono na wangali wanatafuna vinono, na kufaidika na pombe za bure licha ya umri wao kusonga.

Katika mahojiano ya kipekee na mmoja wao mpakani Isebania Kaunti ya Migori, alisema 2023 ni mwaka wake wa 13 na kabla ya hapa aliwahi kuishi Nakuru na Nairobi

Alitetea makahaba wakongwe akisema ndio wenye ujuzi mkubwa inapokuja katika suala la mahaba wala hawajaweka pesa mbele.

Juliet Achieng (sio jina halisi) ambaye alidinda kabisa kutupa jina lake kamili, alikiri kufikia sasa anakaribia miaka 50 lakini ndio kama anajihisi msichana mbichi.

Tajriba ya muda huu wote imenifunza namna ya kuelewa mahitaji ya kila mteja ndiposa ninajaribu kila njia kuhakikisha wajukuu wangu nyumbani pia wanafurahia matunda ya jasho langu, akasema.

Kwa upande mwingine anawasimanga makahaba wachanga, akidai kwamba wamekuwa wakichafulia jina sekta ya ukahaba kutokana na tabia za kuwaibia wateja.

Achieng alitufichulia kuwa binti zake wawili kumwachia wajukuu wawili 2018 na kuhamia jijini  Nairobi kwa ajili ya shughuli za kikazi, ameachiwa jukumu zito la kuwanunulia chakula, kuwalipia karo na kwakidhi mahitaji mengine muhimu ya kimsingi.

Anaungama kuwa bado ana mvuto na wateja wengi bado wanammezea mate ndio sababu akaamua kuendelea na kazi ya ukahaba mpaka atakapofikisha umri wa miaka 55 hivi astaafisha biashara hiyo ambayo ni haramu.

Kulingana na Achieng, marafiki zake wengi wameokoka na kuachana na biashara yenyewe, ila anaomba bado kupatiwa muda kwani anajihisi kuwa na nguvu.

“Mara nyingi huwa ninalenga watalii ambao wamekuwa ni wateja wangu waaminifu kwa muda mrefu tangu nilipokuwa msichana mdogo wa miaka 22 na wanapozuru Kenya ni lazima wanipigie simu.”

Kauli yake si tofauti na ya Ann Waithera, si majina yake halisi, anayesema licha ya kutinga miaka 47 ana nguvu kuhudumia wanaume wenye kiu cha mapenzi.

“Nitastaafu nikifikisha miaka 60,” Waithera akasema.

Waithera na Achieng wanasema hawana kazi rasmi, hivyo basi hawana budi ila kuendeleza ajira waliyo na tajriba ya muda mrefu.

Achieng alisema mume wake alimtoroka maisha yalipoanza kuwa magumu na hadi sasa hawajakutana.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Kuna watu hawafurahii kuona jamii ya Mlima Kenya...

Ulanguzi wa watoto washinikiza serikali kufunga vituo vya...

T L