• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
MALEZI KIDIJITALI: Teknolojia haiwezi chukua nafasi ya mzazi kamwe!

MALEZI KIDIJITALI: Teknolojia haiwezi chukua nafasi ya mzazi kamwe!

NA BENSON MATHEKA

KAMA mzazi enzi hizi za dijitali, ni kawaida kuhisi kwamba teknolojia inaongoza familia yako badala ya kuiongoza wewe mwenyewe.

Hii ni kwa sababu ya jukumu kubwa ambalo teknolojia inatekeleza katika maisha ya kizazi cha sasa.

Hata hivyo wataalamu wa malezi wanasema kwamba hizi ni hisia za kawaida za mzazi kuhisi kwamba analemewa na kuwa nyuma huku watoto ,wakikumbatia teknolojia.

“Ukweli wa mambo ni kuwa, ukiwa mzazi uko katika nafasi ya mamlaka kwa maisha ya mtoto wako hata enzi hizi za dijitali. Hakuna mtu au kifaa chochote, apu au kikundi kinaweza kuchukua nafasi yako kama mzazi. Hakuna sauti nyingine inayoweza kuwa na ushawishi zaidi ya yako katika akili na moyo wa mtoto wako,” asema mtaalamu na matafiti wa malezi dijitali Joan Birdstrong, kwenye ushauri alioandika katika tovuti yake.

Wataalamu wanasema wazazi wanapaswa kutambua ukweli kwamba teknolojia imeongeza ujuzi na majukumu muhimu katika kazi ya ulezi sawa na inavyosababisha madhara ya afya ya akili, mwili, mfadhaiko na dhuluma za mtandao zinazowapa wazazi wasiwasi.

“Hii ndiyo sababu mzazi anapaswa kuchukua mamlaka yake ipasavyo katika malezi ili kuepusha mtoto na hatari hizi. Watoto wakiachwa kutekwa na vifaabebe watapotoka na wa kulaumiwa atakuwa ni mzazi,” asema mtaalamu wa malezi Rhoda Karimi.

Anasema wazazi wakiachia watoto kuzama katika mtandao bila kudhibitiwa, huwa wanawaweka katika hatari ya kusombwa na hatari zinaoibuka enzi hizi za dijitali.

  • Tags

You can share this post!

PENZI LA KIJANJA: Epusha mpenzi na marafiki mafisi vilabuni

FATAKI: Mabinti kufuata pesa ni sawa ila wasikae tu ndee...

T L