• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Kuhifadhi chakula bila friji

MAPISHI KIKWETU: Kuhifadhi chakula bila friji

NA PAULINE ONGAJI

HUKU hali ya uchumi ikizidi kuwa ngumu, wengi wanatamani kununua chakula kingi mara moja kama mbinu ya kupunguza gharama.

Hata hivyo, kuna hofu ya chakula hiki kuharibika haswa ikiwa huna friji. Ufanyeje kisiharibike?

•Kuhifadhi vyakula kwa vifaa vilivyotibiwa: Waweza tibu mkebe wa kuhifadhia chakula kwa kuuchemsha kabla ya kupangusa na kuweka mboga na matunda yaliyooshwa na kupanguswa kisha kuyafunika. Unapofanya hivi hakikisha unatoa hewa yote na baadaye kutumbukiza vifaa hivi kwa maji yanayochemka. Hata hivyo mbinu hii sio maarufu sana sasa ikilinganishwa na miaka ya awali. Ni mbinu inayohitaji kiwango kikubwa cha moto kuondoa bakteria zinazoharibu chakula haraka.

•Kuchemsha: Iwapo umenunua nyama au mboga nyingi, waweza chemsha kama mbinu ya kuhifadhi chakula kwa siku kadha. Hata hivyo unapaswa kuwa mwangalifu kwani mbinu hii sio mwafaka iwapo unataka kuhifadhi chakula kwa muda mrefu.

•Kukausha: Hii ni mbinu ambayo hadi sasa inatumika hasa katika sehemu za mashambani katika uhifadhi wa mazao ya shambani kama vile maharagwe na mahindi. Ni mbinu inayohakikisha maji ambayo huchangia uharibifu wa haraka wa chakula, yanaondolewa.

•Kumwagia chumvi: Ni mbinu mwafaka katika uhifadhi wa vyakula vya protini kama vile nyama, kuku na samaki. Kama kukausha, huondoa majimaji kwenye bidha inayohifadhiwa na hivyo kutoa bakteria zinazoongeza uwezo wa kuharibu chakula.

You can share this post!

UJAUZITO NA UZAZI: Kutokwa damu ukiwa mjamzito

MALEZI KIDIJITALI: Daima kinga yashinda tiba!

T L