• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Kuku wa kupaka

MAPISHI KIKWETU: Kuku wa kupaka

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Saa 3

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • kuku 1
  • pilipili mboga 2
  • punje 4 za kitunguu saumu
  • kijiko 1 cha tangawizi iliyokunwa
  • kijiko 1 cha maji ya limau
  • tui la nazi kikombe 1
  • kijiko ½ cha manjano
  • kijiko cha binzari nyembamba iliyosagwa
  • majani ya giligilani
  • mafuta ya kupikia
  • nyanya 3 zilizokatwakatwa
  • kitunguu maji 2
  • pilipili ya kijani kibichi
  • chumvi

Maelekezo

Andaa kuku kwa kuchanganya viungo vyote ili kutengeneza marinade na kuipaka vizuri kwenye kuku.

Weka kwenye jokofu kwa muda wa saa mbili.

Washa ovena yako kwa sentigredi 180 kwa dakika 15.

Paka mafuta kidogo kwenye kuku, kisha uweke kwenye raki ya kuoka. Oka kwa muda wa dakika 30-40.

Wakati huo huo, weka vijiko viwili vya mafuta kwenye sufuria juu ya moto wa wastani. Wakati ni moto, ongeza vitunguu, kaanga kwa muda wa dakika tano.

Ongeza vitunguu, tangawizi na pilipili ya kijani halafu koroga hadi harufu nzuri ianze kuhanikiza. Ongeza nyanya na kupika hadi chakula kiwe laini.

Ongeza binzari, manjano, na chumvi na endelea kukoroga. Ongeza marinade yoyote iliyobaki.

Changanya katika tui la nazi. Punguza moto na mara kwa mara koroga hadi mchuzi uwe mzito.

Weka kuku katika mchuzi wako, nyunyiza maji kidogo. Funika na chemsha kwa dakika tano.

Onja mchuzi, na kisha upambe na majani ya giligilani.

Epua na upakue kwa chochote ukipendacho.

  • Tags

You can share this post!

Je, unafahamu kwamba kuogelea kuna faida tele?

MAPISHI KIKWETU: Muhogo wa nazi

T L