• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
MAPISHI KIKWETU: Muhogo wa nazi

MAPISHI KIKWETU: Muhogo wa nazi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MUHOGO wa nazi ni rahisi sana kuandaa na huwa na ladha nzuri.

Ni chakula ambacho kimepata sana umaarufu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki.

Mlo huu hupikwa katika tui la nazi na chumvi, pilipili ya kijani na tangawizi kidogo.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 3

Vinavyohitajika

Mihogo mibichi. PICHA | MARGARET MAINA
  • mihogo 6, ichonge na uikate vipande vipande
  • chumvi
  • kijiko 1 cha pilipili ya kijani
  • kijiko 1 cha tangawizi
  • nazi 1 mbichi
  • vikombe 4 vya maji

Maelekezo

Para nazi. Weka nazi iliyokunwa kwenye kimiminiko na maji kiasi cha kati ya kikombe 1-1½. Ichakate.

Weka mchanganyiko katika kichungi na ufinye ili kupata tui la nazi. Sasa una tui nene la nazi. Weka kando hadi utakapohitaji.

Rudisha nazi kwenye blenda. Ongeza vikombe 2 vya maji na uchanganye tena.

Osha na ukate mihogo vipande vipande.

Weka vipande vya mihogo, tui la nazi, pilipili, chumvi na tangawizi kwenye sufuria iliyoinjikwa kwa chanzo cha moto.

Ruhusu mihogo iive kwa moto mdogo hadi wa wastani. Koroga mara kwa mara ili mihogo isishikamane chini ya sufuria.

Ikiwa ni lazima, unaweza kuongeza maji kidogo.

Mihogo ikiiva na mchanganyiko kuwa mzito kidogo, epua, changanya na upakue ili ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Kuku wa kupaka

Faida za matunda aina ya pepino melon

T L