• Nairobi
 • Last Updated February 26th, 2024 9:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Mboga na korosho za kukaangwa

MAPISHI KIKWETU: Mboga na korosho za kukaangwa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 2

Vinavyohitajika

 • kikombe ½ korosho
 • kikombe 1 hisa ya kuku
 • karoti 1
 • zukini 1
 • mbaazi kikombe 1 yaliyochemshwa
 • kikombe 1 cha maharagwe yaliyochemshwa
 • kikombe 1 cha karanga
 • mahindi tamu kikombe ½
 • kitunguu maji 2
 • kikombe ½ koliflawa
 • brokoli kikombe ½
 • wali uliochemshwa vikombe 2

Maelekezo

Kata mboga zote. Jaribu kutoacha vipande vikiwa vikubwa sana kwani havipikiki haraka vikiwa hivyo.

Injika sufuria ya kukaanga kwenye chanzo cha moto wa kati. Ongeza hisa ya kuku na uache ipate moto kidogo.

Ongeza korosho, karoti iliyokatwakatwa vizuri, koliflawa na brokoli. Koroga ili kuchanganya na kufunika katika hisa ya kuku na uache hivi viive kwa muda wa dakika mbili.

Kisha ongeza viungo vingine isipokuwa wali. Koroga ili kuchanganya viungo na hisa kuenea juu ya viungo vyote.

Pika kwa muda wa dakika tano na kisha ongeza wali na upike hadi mboga ziwe tayari kuliwa. Koroga mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa haishiki kwenye sufuria na kuungua.

Pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

Mbolea nafuu yatekwa na mabroka Kakamega

Ruto atuza wafuasi bila mahasla halisi

T L