• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Sweet and sour chicken

MAPISHI KIKWETU: Sweet and sour chicken

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 15

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • kuku 1 ½ bila mifupa, kata vipande vipande
  • kikombe ¼ cha wanga
  • mayai 2
  • kikombe ¼ cha unga ngano
  • mafuta ya kanola kukaangia
  • vipande vya nanasi kikombe 1
  • pilipili mboga ya rangi nyekundu; kata vipande vipande
  • kitunguu maji 2
  • kikombe ¼ cha sukari
  • kikombe cha sukari ya kahawia
  • kikombe cha siki ya tufaha
  • kikombe ¼ ketchup
  • vijiko 4 sosi ya soya
  • karafuu kikombe ½
  • kitunguu saumu punje 6

Maelekezo

Ili kufanya mchuzi, changanya sukari, sukari ya kahawia, ketchup, sosi ya soya na vitunguu kwenye kijibakuli.

Mimina mafuta ya kanola kwenye kikaangio, pasha mafuta juu ya chanzo cha moto wa wastani.

Ongeza wanga wa mahindi kwenye mfuko mkubwa kisha ongeza vipande vya kuku kwenye mfuko huo na utikise mpaka vipande vyote vijipake wanga vizuri.

Chukua vipande vya kuku uviweke ndani ya yai ulilopasua na kukoroga, kisha ndani ya unga kabla ya kutumbukiza kwenye mafuta ya moto.

Pika kuku kwa dakika tano hadi minofu hiyo iwe na rangi ya kahawia. Epua.

Kwenye kikaangio hicho tu, ongeza pilipili mboga, vitunguu na vipande vya nanasi na upike kwa dakika mbili, hadi viwe laini.

Ongeza sosi ya soya tena na ukoroge na ufunike kwa dakika mbili.

Ongeza vipande vya kuku tena na koroga hadi mchuzi uwe mzito na unabubujika. Ongeza korosho na uache kwa dakika tano kisha epua.

Pakua na ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

PAUKWA: Uchungu wa mwana aujuaye mama mzazi

MWALIMU WA WIKI: Iwapo ni siri ya ufanisi tu, hii hapa

T L