• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:10 PM
MAPISHI KIKWETU: Wali mwekundu kwa samaki

MAPISHI KIKWETU: Wali mwekundu kwa samaki

NA PAULINE ONGAJI

Viungo

Mchele vikombe – 2

Samaki mkubwa vipande vinne

Mafuta ya kukaanga lita – ¼

Vitunguu vikombe – 1 ½

Kitunguu saumu kijiko 1 ½

Bizari kijiko cha chai – ¼

Nyanya zilizomenywa vikombe – 2

Mchuzi wa nyama – 2

Tui la nazi vijiko vya meza – 2

Siki ya ndimu kikombe – ½

Maji kikombe – 2

Jinsi ya kutayarisisha

  1. Kwenye bakuli kubwa changanya siki ya ndimu kikombe ½ na maji kikombe kimoja.
  2. Ongeza kitunguu saumu kijiko ½ pilipili na chumvi kwenye mchanganyiko. Ukitumia mwiko wa mbao koroga hadi viungo vyote vichangamane.Tia mapande ya samaki kwenye mchanganyiko na uchanganye. Yafunike kisha usubiri kwa kati ya dakika 15 – 20 ili viungo vikolee kwenye samaki.
  3. Kwenye sufuria, tia mafuta ya kukaanga vijiko vya meza 3 huku kiasi cha moto kikiwa cha kiwango cha kati.
  4. Ongeza kikombe 1 cha vitunguu, kitunguu saumu na bizari kisha uvikaange huku ukikoroga kwa utaratibu kwa dakika chache hadi vitunguu vinyooke na mafuta yakolee kwenye mchanganyiko.
  5. Ongeza nyanya kikombe 1 na chumvi. Punguza kiasi cha moto hadi kiwango cha chini. Koroga kwa utaratibu hadi nyanya ziive na kuwa nyororo.
  6. Funika mchanganyiko kwa dakika 10. Tia vijiko viwili vya tui la nazi mchuzi wa nyama au kuku na mchele katika mchanganyiko. Koroga kikamilifu kwa utaratibu kisha upunguze kiasi cha moto hadi kiwango cha chini.
  7. Kwenye karai, kaanga samaki hadi pande zote za zibadili na kuwa rangi ya hudhurungi. Andaa.
  • Tags

You can share this post!

UJAUZITO NA UZAZI: Ishara za ‘nasal polyps’ kwa mtoto

Waiguru atetea serikali kuhusu mgao wa kaunti

T L