• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
MAPISHI KIWETU: Firigisi ya kuku

MAPISHI KIWETU: Firigisi ya kuku

NA MARGARET MAINA

[email protected]

FIRIGISI ni sehemu ya mfumo wa mmeng’enyo wa kuku.

Kwa kuwa kuku hawana meno, wanahitaji njia nyingine ya kuvunja chakula chao ili kiwe rahisi kumeng’enyeka. Kazi hiyo hufanywa na firigisi.

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • kilo 1 ya firigisi safi
  • kitunguu maji kilichokatwa
  • majani ya bay
  • punje 5 za kitunguu saumu
  • nyanya 2
  • kijiko ¼ paprika
  • bizari ya kuku
  • kijiko ¼ jira
  • kijiko ¼ pilipili nyeusi
  • kijiko ½ manjano
  • chumvi
  • maji ya kuchemsha
  • pilipili
  • mafuta ya kupikia
Firigisi ya kuku ikiwa mbichi. PICHA | MAKTABA

Maelekezo

Kwa kuwa firigisi ni misuli, ni ngumu sana. Kwa hivyo kabla ya kufanya chochote nayo, ni muhimu uifanye iwe laini.

Jaza sufuria na maji na uongeze majani matatu ya bay. Tumbukiza firigisi.

Weka sufuria kwenye moto na uache firigisi ichemke kwa muda wa hadi saa moja hadi saa moja na nusu au firigisi iwe laini.

Epua na uondoe kwenye supu. Wacha ipoe.

Mara tu firigisi ikishapoa kidogo baada ya kulainika, ihamishe kwenye ubao wa kukata na ukate vipande vidogo. Pia, osha na usage punje za kitunguu saumu.

Kwenye sufuria ya kina, ongeza mafuta na kitunguu saumu (usisubiri mafuta yapate moto, ongeza kitunguu saumu mara tu baada ya kuongeza mafuta kwenye sufuria), ongeza paprika, bizari ya kuku, jira, pilipili nyeusi na manjano.

Koroga na kaanga kitunguu kwenye moto wa kati kwa dakika kadhaa, kisha ongeza pilipili.

Ongeza vikombe 1.5 vya maji ya moto na koroga, kisha ongeza firigisi na ukoroge ili kufunika na mchuzi.

Ongeza chumvi, funika sufuria, na upike kwa muda wa dakika 20 juu ya moto wa kati.

Baada ya dakika 20, onja na urekebishe viungo unavyotaka, kisha upike kwa dakika 10 zaidi kabla ya kuondoa sufuria kutoka kwa moto.

Epua na pakua kwa chochote upendacho.

Sasa ni muda mwafaka wa kufurahia mlo wako.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Ugonjwa wa matumbwitumbwi unavyoathiri watu...

Rennes waangusha miamba PSG katika Ligi Kuu ya Ufaransa

T L