• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
DKT FLO: Kwa miezi 3 sasa koo yanisumbua

DKT FLO: Kwa miezi 3 sasa koo yanisumbua

Nimekuwa nikikumbwa na maumivu ya koo kwa miezi mitatu sasa. Licha ya ya matibabu sijashuhudia mabadiliko. Je, hii yaweza kuwa dalili ya kansa ya koo?

S.L, Mombasa

Mpendwa S.L,

Kukumbwa na maumivu ya koo kwa mwezi mmoja yaweza tokana na maambukizi ambayo hayajatibiwa. Aidha, huletwa na mwasho unaotokana na kamasi puani au sinusitis inayosababisha kutiririka kwa kamasi kwenye koo pengine kutokana na mzio au maambukizi (sinus infection).

Maumivu ya koo pia yaweza kuwa ni kutokana na chakula tumboni kupanda juu hadi kwenye umio (oesophagus), na hivyo kusababisha mwasho katika sehemu hii, na wakati mwingine kuenda hadi kwenye njia ya kupitisha hewa (reflux).

Kukaukiwa, kutaabika kutoa sauti, kukohoa kwa muda mrefu na kusafisha koo, aidha ni baadhi ya mambo ambayo yaweza sababisha maumivu ya koo.

Unashauriwa kutafuta ushauri wa mtaalamu wa ENT ili ufanyiwe uchunguzi wa koo. Matibabu yatategemea na kinachosababisha tatizo lako, kwa mfano, mzio unatibiwa kwa kutumia anti-histamines; viua vijasumu hupendekezwa kutibu maambukizi yoyote; dawa maalum ya kunyunyiza puani (nasal spray) yaweza tumika kuzibua mfumo wa sinuses na dawa za kupunguza viwango vya asidi tumboni.

Aidha, kunywa kati ya glasi 6 na 8 za maji ili kuepuka tatizo la kutaabika kutoa sauti, vilevile kusafisha koo yako kila mara.

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Je, bora mitishamba?

MUME KIGONGO: Gauti: Itakubidi kupunguza pombe na nyama...

T L