• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Hii ndio picha halisi ya Siku ya Kiyaama – Sehemu 2

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Hii ndio picha halisi ya Siku ya Kiyaama – Sehemu 2

NA HAWA ALI

SIFA zote njema anastahiki Mola Azzawajalla, swala na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad.

Awali tulizungumza kuhusu picha halisi ya Siku ya Kiyaama, na leo Mungu akipenda tuendeleze mada hiyo.

Siku hiyo, hukumu itatolewa katika ardhi iliyo tambarare kabisa ambapo viumbe vyote vitahudhurishwa. Malaika wote watasimama katika safu: “Siku ambayo zitasimama Roho (za viumbe wote) na Malaika safu safu; hatasema siku hiyo ila yule ambaye (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema amempa idhini ( ya kusema) na atasema yaliyo sawa”. [78:38]

Kisha kiti cha Enzi cha Allah (s.w.) cha kutolea Hukumu kitahudhurishwa pale na Nuru Yake itazagaa kila mahali na kila mmoja atakuwa na uhakika kuwa Allah (s.w.) yupo kwa kuchukua Hisabu. Qur’an tukufu inatupa picha ya Siku hiyo kuwa:

Na ardhi (siku hiyo) itang’ara kwa nuru ya Mola wake, na madaftari (ya vitendo) yatawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi na kutahukumiwa baina yao kwa haki wala hawatadhulumiwa”. [39:69]

Kila mmoja atapita katika hisabu, japo wengine hisabu zao zitakuwa ngumu sana na wengine nyepesi sana. Hebu tuzingatie Hadith zifuatazo: Aysha amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.w.) amesema: Yeyote atakayehisabiwa (atakayeulizwa) katika siku ya Hukumu, ataangamia. Nikauliza (Aysha) Je, Allah hakusema: “Basi Yeye Atahisabiwa hisabu nyepesi?” [84:8] Akajibu: Hayo kwa hakika ni maelezo ya ujumla lakini atakayehisabiwa kila kitu kwa undani wake, ataangamia. [Bukhari na Muslim]

Hadith inatufundisha kuwa kila mmoja atahisabiwa, lakini yule ambaye hisabu yake haitafanywa nyepesi, hataweza kufaulu kutokana na maelezo yake na bila shaka atakuwa ni mtu wa motoni. Pia Hadith ifuatayo inasisitiza juu ya kila mtu kuulizwa na Allah (s.w.):

Mtume Muhammad amesema, Hapana yeyote kati yenu ambaye hataongea na Mola wake.

Hapatakuwa na mkalimani yeyote kati ya Allah na yeye na hapatakuwa na pazia ya kumzuia Allah asionekane. Mja ataangalia kuliani kwake, lakini hatoona chochote isipokuwa matendo yake aliyoyatanguliza.

Ataangalia mbele yake, lakini hataona chochote isipokuwa moto unaomjia usoni mwake. Kwa hiyo jikinge na moto(na kutoa sadaka) angalau kipande cha tende. [Bukhari na Muslim] Vile vile tunafahamishwa katika

1. Ujana wako umeutumiaje?

2. Umri wako umeutumiaje?

3. Mwili wako na vipaji vyako umevitumiaje?

4. Mali yako umeipataje na umeitumiaje?

5. Elimu yako umeitumiaje ?

Maswali haya yataulizwa mbele ya viumbe vyote vilivyoumbwa tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka mwisho wake. Kila mchunga (kila kiongozi katika ngazi yoyote ile) ataulizwa juu ya uchungaji (uongozi) wake.

Mitume ndio watakaokuwa wa kwanza kuulizwa. Allah (s.w.) atawauliza Mitume: Ni lipi jibu lenu. Watajibu: Hatuna ujuzi. Hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa siri (ghaibu)”.

You can share this post!

FIDA yahimiza wapigakura kuchagua wanawake kuongeza idadi...

Balala avunja kimya, aidhinisha Mung’aro kwa ugavana...

T L