• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Mfanyabiashara anayenunua mende na kunguni Nakuru

Mfanyabiashara anayenunua mende na kunguni Nakuru

RICHARD MAOSI NA DILIGENCE ODONGO

MKAZI kutoka Nakuru amewashangaza watu kwa kununua mende na kunguni kutoka kwa wenyeji, ‘biashara’ ambayo imeonekana kumzolea umaarufu anapohamasisha uuzaji wa wadudu hao.

Aidha, kwa kila mdudu au kimelea hununua Sh5.

Katika pitapita zetu katikati ya jiji la Nakuru, tunakutana na kundi la watu wamezingira kibanda chake akiendelea kuwapatia maelezo namna ya kuimarisha usafi nyumbani.

Kwa ujasiri mkubwa, Mzee Stephen Mwangi akiwa amebeba chombo cha glasi kilichojaa mende na kunguni, anaendelea kuwahudumia wateja ambao baadhi wamekuja kununua dawa za kuua wadudu, huku wengine wakishuhudia sinema ya bure.

Mwangi anasimamia mauzo katika Ukanda wa Bonde la Ufa akiwa mmoja wa maafisa wa mauzo.

Katika mahojiano ya kipekee na Taifa Leo Dijitali, anasema hutumia wadudu kutangaza dawa ya One touch ambayo hutumika kuwaangamiza.

Anasema amekuwa akifanya kazi ya kutoa matangazo ya biashara na alipopata fursa ya kutoa maelezo ya dawa za kuangamiza wadudu ya One Touch, aliamua kutumia njia ambayo sio ya kawaida.

Mwangi anasema hili ni wazo ambalo alivumbua yapata miaka miwili iliyopita, ikizingatiwa kuwa biashara inahitaji ubunifu ili kuvutia wateja.

Taifa Leo Dijitali ilipotaka kujua anakotoa kunguni na mende, alisema kuna kundi maalum la vijana kutoka Nairobi ambao wamepatiwa kibarua cha kukusanya wadudu ambao hatimaye husafirishwa hadi jijini Nakuru kwa njia ya bahasha – parcel.

Akizungumza na wateja waliokuwa wamezingira kibanda chake, anaungama kuwa hununua mende na kunguni kwa Sh5 kila moja.

“Kwa kweli huwa sipotezi muda nikiskia kuwa kuna mtu ambaye yuko tayari kuuza mende na kunguni,” akasema.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Waliohadaa mfanyabiashara Sh5.4 milioni wakidai...

Atwoli achaguliwa tena kama Rais wa Muungano wa Vyama vya...

T L