• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Mulamwah arejea Milele FM siku chache baada ya kuondoka

Mulamwah arejea Milele FM siku chache baada ya kuondoka

MWANDISHI WETU

MCHESHI David Oyando almarufu Mulamwah amerejea katika stesheni ya Milele FM, siku chache baada ya kutangaza kuacha kazi na kuondoka.

Kupitia ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Mulamwah alisema kuwa amerejea kazini na atakuwa kwenye shoo yake kila wiki kama ilivyokuwa desturi.

“Nimerudi Milele FM, tulikuwa na mazungumzo kadhaa na tukafikia uamuzi mmoja. Mambo iko safi kabisa!! Shoo Konki yaendelea saa saba hadi saa kumi – Jumatatu hadi Ijumaa. Asanteni sana wafuasi wangu,” akasema.

Kairbu wiki moja iliyopita, mcheshi huyo aliandika kuwa ameondoka katika stesheni hiyo baada ya kutoelewana na wasimamizi wa redio hiyo.

Mulamwah alisema kuwa aliwacha kazi baada ya mwaka mmoja na miezi mitatu ya utendakazi.

“Hatukuelewana kuhusu sehemu zingine za mkataba na upeo wa kazi ndio maana nimewacha kazi,” akaeleza.

Mapema wiki hii, mtangazaji maarufu wa stesheni hiyo Alex Mwakideu alitangaza kuondoka kwake, lakini akabadilisha nia saa chache baadaye.

Mwakideu ambaye alijiunga na kituo hicho cha redio 2018 alisema kuwa aliamua kufunganya virago vyake baada ya kutoelewana na mwajiri wake.

“Asanteni sana kwa simu na jumbe zenu, tulikuwa tumevurugana kidogo lakini yote yamesuluhishwa,” akaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Raila: Askari waliangamiza watu 72 wakati wa maandamano

Maafisa chonjo baada ya Al-Shabaab kutekeleza mashambulio...

T L