• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 3:13 PM
MUME KIGONGO: Japo kitambi kina madhara tele kiafya, kina faida zake pia

MUME KIGONGO: Japo kitambi kina madhara tele kiafya, kina faida zake pia

NA LEONARD ONYANGO

TOFAUTI na wanawake ambao huhifadhi mafuta ya ziada mwilini kwenye mapaja, kiuno na makalio, wanaume huyahifadhi tumboni.

Hiyo ndiyo maana wanaume wanaokula sana au kubugia pombe kupita kiasi bila kufanya mazoezi, huwa na tumbo kubwa.

Wataalamu wanaonya kuwa ni vigumu kumaliza mafuta yanayosababishwa na pombe hata mwathiriwa akifanya mazoezi. Mafuta yanayosababishwa na pombe (visceral fat) huzunguka viungo kama vile moyo hivyo kuwa vigumu kuyamaliza kwa mazoezi tu – bali mwathiriwa anahitaji kubadili lishe pia.

Japo mafuta mengi tumboni yamehusishwa na maradhi kama vile kisukari, ugonjwa wa moyo, matatizo ya kibofu cha mkojo, kiharusi (stroke) kati ya magonjwa mengineyo, tafiti zinaonyesha kuwa kitambi kina manufaa pia.

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Erciyes nchini Uturuki, inaonyesha kuwa wanaume wenye tumbo kubwa ‘wanashibisha’ wapenzi au wake zao kitandani ikilinganishwa na wasio na kitambi.

Utafiti huo ulidai kuwa madume wenye vitambi wanadumu kwenye tendo kwa muda mrefu.

Wataalamu hata hivyo, wanaonya kuwa madhara ya mafuta mengi tumboni ni makubwa zaidi kuliko faida.

Tumbo kubwa limehusishwa na udhaifu wa mbegu za kiume. Hiyo inamaanisha kuwa watu wenye vitambi wanakabiliwa na hatari ya kushindwa kutungisha mimba.

Wataalamu wanaonya kuwa wanaume wenye matumbo makubwa wako katika hatari ya kufariki mapema ikilinganishwa na wenzao ambao ni wembamba kwa sababu wanaandamwa na msururu wa magonjwa.

Wanasayansi wanashauri kuwa mbali na mazoezi kuna njia nyingine za kiasili mwathiriwa anaweza kutumia kupunguza mafuta tumboni.

Vyakula vya protini vinasaidia kupunguza hamu ya kula hivyo kukuwezesha kula kiasi kidogo cha chakula. Kuepuka pombe, nafaka zilizokobolewa na kuketi kwa muda mrefu; kunaweza kusaidia kupunguza mafuta tumboni.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Selimundu huua watoto 10,000 nchini Kenya...

JIJUE DADA: Kukabili tatizo la upele na mwasho kwenye...

T L