• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Mwenyekiti wa Azimio Nakuru alalamikia waandamanaji kuiba sabuni  

Mwenyekiti wa Azimio Nakuru alalamikia waandamanaji kuiba sabuni  

NA SAMMY WAWERU

MWENYEKITI wa Azimio la Umoja tawi la Nakuru Mashariki, Maina Kairu amekashifu vikali maandamano ya upinzani katika kaunti akilalamikia uharibifu wa mali na biashara. 

Kwenye kikao na wanahabari mnamo Jumapili, Julai 23, 2023 Bw Kairu alitoa mfano wa wizi wa sabuni wakati wa maandamano ya Azimio, akitaja hatua hiyo kama inayolenga kugeuza jamii kuwa maskini.

“Nashangaa eneo kama Nakuru Magharibi, baadhi ya waandamanaji walionekana wakiiba sabuni. Ni aibu iliyoje?” alihoji afisa huyo.

Akijitenga kushiriki maandamano ya upinzani yaliyoitishwa na kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, Bw Kairu alisema yeye anaunga mkono serikali ya sasa inayoongozwa na Rais William Ruto.

Afisa huyo alisema Kenya Kwanza imemthibitishia kuwa na uwezo kubadilisha uchumi wa taifa kuwafaa wananchi.

“Tumeona waandamanaji wengine wakiiba hata chakula. Hiyo ni sera ya kuletea jamii umaskini,” Kairu alisema, akisuta wanaoshiriki maandamano. 

Aidha, alisema haogopi kuvuliwa wadhifa wake akipendekeza endapo atapatikana hafai chamani basi unaweza kupokezwa kiongozi mwingine. 

“Niliitwa kikao na wazee, wakanihimiza kuzungumza na wafuasi wangu kukoma kushiriki maandamano.”

Bw Kairu alieleza nia yake kutaka kushirikiana na serikali ya kaunti ya Nakuru na ya kitaifa. 

Azimio imeitisha maandamano kushinikiza serikali kushusha gharama ya maisha. 

  • Tags

You can share this post!

Bondia Wanyonyi adhihirisha Kenya imara kwa kumtandika...

Ruto awataka viongozi wa Azimio kutuma watoto wao kuongoza...

T L