• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Ruto awataka viongozi wa Azimio kutuma watoto wao kuongoza maandamano

Ruto awataka viongozi wa Azimio kutuma watoto wao kuongoza maandamano

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto amewakashifu vikali vinara wa Azimio la Umoja, akiwataka watumie wanao kuongoza maandamano ya upinzani. 

Akizungumza Jumapili, Julai 23, 2023 baada ya kushiriki ibada ya kanisa katika Kaunti ya Taita Taveta, kiongozi wa nchi alisikitikia wanasiasa kutumia watoto wa watu kulumbana na serikali.

“Haiwezi kuwa watoto wako unawachunga, lakini wa wengine unawapiganisha na askari,” Rais Ruto akasema.

Matamshi hayo yalionekana kuelekezewa viongozi na wanasiasa wa Azimio, kufuatia msimamo wao mkali kuendeleza maandamano ya siku tatu kila wiki kushinikiza serikali kushusha gharama ya maisha.

Dkt Ruto aidha alilalamikia maafisa wa polisi kujeruhiwa wakati wa maandamano.

Wiki iliyopita, Azimio ilizindua awamu ya kwanza ya maandamano ya siku tatu askari wakimenyamana na waandamanaji.

“Tuna askari wengi wameumia, wako hospitalini,” Rais Ruto alisema, akikashifu waandalizi wa maandamano hayo.

Kinara wa Azimio, Raila Odinga licha ya kutoonekana wiki iliyopita alisisitiza kuwa upinzani hautalegeza kamba jitihada kusukuma serikali kuangazia masuala yanayokumba Wakenya, ikiwemo kushusha gharama ya juu ya maisha.

Serikali imeharamisha maandamano, ikitoa onyo kali kwa wahusika.

Visa kadha vya maafa yanayotokana na washirika kupigwa risasi na polisi vimeripotiwa, na pia kadha kujeruhiwa vibaya.

Huku askari wakinyooshewa kidole cha lawama, Rais Ruto amewapongeza kwa kile anahoji ni “kusaidia kuzuia vifo kutokea, uharibifu wa mali na biashara”.

Analalamikia hatua ya upinzani kuandaa maandamano, akihoji unalenga kulemaza jitihada zake kukuza taifa.

“Wanasiasa, licha ya tofauti zetu tusishiriki kuharibu nchi yetu.”

  • Tags

You can share this post!

Mwenyekiti wa Azimio Nakuru alalamikia waandamanaji kuiba...

Yaya mshukiwa wa wizi wa watoto Nakuru akamatwa Nairobi

T L