• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 2:11 PM
Namna tofauti za kukabili maumivu ya kichwa

Namna tofauti za kukabili maumivu ya kichwa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

PAMOJA na sababu za kawaida kama vile kuwa na mafua, kutokunywa maji ya kutosha na mfadhaiko, pia kuna sababu zaidi za kuumwa na kichwa kama vile matatizo ya kulala, kunywa pombe kupita kiasi na matumizi ya kupita kiasi ya dawa za kutuliza maumivu.

Zipo njia za kiasili zinazotumika kupunguza maumivu ya kichwa.

Ikiwa unasumbuliwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara, kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kununua dawa dukani kwa haraka.

Kuna dawa mbadala za kiasili za maumivu ya kichwa, ambazo zimethibitishwa kusaidia kutibu maumivu ya kichwa haraka.

Ikiwa una wasiwasi kuwa unaumwa na kichwa zaidi ya kawaida, basi hakikisha unamtembelea daktari ili kuangalia kila kitu kiko sawa.

Menthol yenye harufu ya sintetiki iliyotengenezwa na mnanaa na inaweza kusaidia kutibu maumivu ya kichwa.

Masaji kwa mkono wako (au hata bora zaidi, pata mtu mwingine akufanyie) katika sehemu yenye nyama katikati ya kidole gumba na kidole cha mbele. Inaaminika kuwa una eneo la acupressure hapa ambalo linahusiana na kichwa na kupunguza mvutano hapa kutasaidia kupunguza maumivu ya kichwa chako.

Fukiza ukungu baridi kichwani kupunguza maumivu ya kichwa.

Chumvi ya Himalaya inaweza kutibu maumivu ya kichwa. Inahusisha matumizi ya juisi ya limau, maji ya moto na vijiko viwili vya chumvi ya Himalaya.

Njia nzuri ya kuondoa maumivu ya kichwa haraka, kwani maumivu ya kichwa yanaweza kuletwa na misuli iliyogandamana kwenye shingo yako na kichwa, ni kushikilia chupa ya maji ya moto kwenye paji la uso wako na nyuma ya shingo yako. Kufanya hivyo kunapumzisha misuli na kupunguza maumivu.

Masaji kwa utaratibu kichwa chako ili kuondoa haraka maumivu ya kichwa.

  • Tags

You can share this post!

Barcelona waafikiana na Bayern kuhusu uhamisho wa Robert...

Kidero akosesha Wanga usingizi kuhusu ugavana

T L