• Nairobi
  • Last Updated September 26th, 2023 10:25 PM
Namna ya kulikabili tatizo la kutokwa na damu puani

Namna ya kulikabili tatizo la kutokwa na damu puani

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KUTOKWA na damu puani ni jambo la kawaida. Pua ina mishipa mingi ya damu, ambayo iko karibu na uso mbele na nyuma ya pua.

Mishipa hii ni dhaifu sana na huvuja damu kwa urahisi.

Kulingana na zahanati ya Mayo Clinic, kuna sababu nyingi za kutokwa na damu puani. Kutokwa na damu kwa pua kwa ghafla mbaya sana. Lakini ikiwa una tatizo hili mara kwa mara, unaweza kuwa na tatizo kubwa zaidi inakulazimu upate ushauri wa daktari.

Hewa kavu ndio sababu ya kawaida ya kutokwa na damu kwenye pua. Kuishi katika eneo lenye hewa kavu kunaweza kusababisha utando wa pua kukauka. Huo utando ni tishu ndani ya pua.

Ukavu huu husababisha ukoko ndani ya pua. Kukausha kunaweza kuwasha au kuwashwa. Ikiwa pua yako imekunwa au kuchunwa, inaweza kutoa damu.

Kumeza antihistamini na dawa za kupunguza mzio, na mafua, hukausha utando wa pua na kusababisha kutokwa na damu puani. Kupuliza pua mara kwa mara ni sababu nyingine ya kutokwa na damu ya pua.

Unaweza kujaribu kujitibu nyumbani. Wakati umekaa, jaribu kufinya sehemu laini ya pua yako.

Hakikisha kwamba mianzi ya pua imefungwa kabisa. Ifinye pua kwa dakika 10, inama mbele kidogo, na pumua kupitia kinywa chako.

Usilale chini unapojaribu kuzuia kutokwa na damu puani. Kulala chini kunaweza kusababisha kumeza damu. Baada ya dakika 10 angalia ikiwa damu imekoma. Rudia hatua hizi ikiwa damu inaendelea.

Unaweza pia kutumia vibana baridi juu ya daraja la pua yako au kutumia dawa ya kunyunyizia pua ili kufunga mishipa midogo ya damu.

Muone daktari wako mara moja ikiwa huwezi kuacha kutokwa na damu puani peke yako. Unaweza kuwa na tatizo ambayo inahitaji matibabu zaidi.

Kuna njia kadhaa za kuzuia kutokwa na damu kwenye pua

Tumia chombo cha unyevu ndani ya nyumba yako ili kuweka unyevu hewani.

Epuka ‘kuchokora’ pua yako.

Punguza utumiaji wako wa aspirini,j adili hili na daktari wako kwanza.

Tumia antihistamini na dawa za kupunguza mzio kwa kiasi. Hizi zinaweza kukausha pua.

Tumia dawa ya chumvi au jeli ili kuweka unyevu kwenye pua.

  • Tags

You can share this post!

Wawili wajeruhiwa Mukuru kwa kupigwa na stima

Athari za ukosefu wa maji mwilini

T L