• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
NGUVU ZA HOJA: Dhima ya tafsiri katika kukuza fasihi na kupanua mwonoulimwengu

NGUVU ZA HOJA: Dhima ya tafsiri katika kukuza fasihi na kupanua mwonoulimwengu

NA PROF IRIBE MWANGI

JUMAMOSI iliyopita niliwasiliana na rafiki ambaye pia ni mwanafunzi wangu wa zamani Hezekiel Gikambi.

Aliniarifu kuwa alibahatika sana ‘kuwa miongoni mwa wasomaji wa kwanza wa Mualkemia (riwaya ambayo) ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu cha mwandishi maarufu (kutoka Brazili), Paulo Coelho, The Alchemist.’

Gikambi aliendelea kufafanua kuwa Ali Attas alifanya kazi nzuri ya kukitafsiri kitabu hicho ambacho kwanza kiliandikwa kwa Kireno.

Aidha, Attas amefanya Kiswahili kiwe kati ya lugha 88 ambazo vitabu vya Paulo Coelho vimefasiriwa kwanzo.

Kwa maoni yake, hili ni tukio la kihistoria hasa ikizingatiwa kwamba zaidi ya nakala milioni 320 za mwandishi huyu zimeuzwa. Kiswahili sasa, kupitia kwa tafsiri hii, kipo katika ujirani mzuri!

Brazil, nchi ya mwandishi, ni mbali sana na Kenya. Tafsiri hii inanikumbusha tafsiri za kazi kama vile Animal Farm (Shamba la Wanyama) cha Geroge Orwel, The Government Inspector (Mkaguzi Mkuu wa Serikali) cha Nikolai Gogol na Julius Caesar (Julias Kaizari) na The Merchants of Venice (Mabepari wa Venisi) vya William Shakespear. Hizi pia ni kazi muhimu lakini zinazoashiria umbali wa kimasafa na kiwakati.

Hata hivyo, tunajifunza tamaduni fulani za Brazil kutoka kwa Coelho kama ambavyo tunajifunza za Urusi kutoka kwa Gogol na za Uingereza kutoka kwa Shakespeare na Orwell.

Tafsiri basi hutujuza tamaduni ngeni ziwe zinahusu uchumi, siasa au jamii tu. Tafsiri pia hupanua mwonoulimwengu wa msomaji na kumruhusu kujumuika na ulimwengu hasa wakati huu wa utandawazi. Zaidi ya yote, tafsiri ya fasihi huburudisha huku ikifunza.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Nafasi ya viongozi katika ukuzaji wa lugha...

KAULI YA MATUNDURA: Tufanye nini kwenye hafla ya...

T L