• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
KAULI YA MATUNDURA: Tufanye nini kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani mwezi ujao?

KAULI YA MATUNDURA: Tufanye nini kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani mwezi ujao?

NA BITUGI MATUNDURA

MNAMO Julai 7, 2022, ulimwengu mzima utaadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani.

Hii itakuwa hafla ya kwanza tangu Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) litangaze tarehe hiyo kwenye kikao chake cha 41 mjini Paris, Ufaransa mwaka 2021.

Kiswahili ni mojawapo ya lugha zenye wasemaji wengi kusini mwa Jangwa la Sahara – mbali na kuwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa sana ulimwenguni. Takriban zaidi ya watu milioni 200 huzungumza Kiswahili kote duniani.

Julai 7 iliteuliwa na UNESCO kwa msingi kwamba, ni siku hiyo, mnamo 1954 ambapo chama cha Tanganyika African National Union (TANU) – kikiongozwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania aliidhinisha Kiswahili kuwa lugha ya kuwaunganisha Watanganyika katika harakati za kuikomboa nchi hiyo kutokana na nira ya ukoloni.

Mwanzilishi wa taifa la Kenya, hayati Mzee Jomo Kenyatta wa Kenya – vile vile alitumia mwito wa ‘Harambee’ kuwarai Wakenya kuungana ili wakabili ukoloni. Isitoshe, mnamo Julai 7, 2000, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ilifufuliwa ili kuvuvia tanuri ya ushirikiano wa nchi za ukanda huu – zikiwemo Rwanda, Burundi na Sudan Kusini, ambapo Kiswahili kina wazungumzaji wengi.

Juma lililopita, mshairi na mwanaharakati – Ustadh Abdilatif Abdalla alinipigia simu na kuniuliza: “Kenya imeweka mikakati gani ya kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani?”

Mtaalamu, Prof Kimani Njogu anahisi kwamba tofauti na Tanzania ambapo Serikali hufadhili masuala yanayohusu Kiswahili, Kenya itategemea mno juhudi za watu binafsi kufanikisha maadhimisho ya siku hiyo.

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Dhima ya tafsiri katika kukuza fasihi na...

Kane atoa pumzi Ujerumani, Italia ikimumunya Hungary

T L