• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 10:55 AM
NGUVU ZA HOJA: Mabunge ya Kenya yatuzwa na chama cha CHAUKIDU kwa kustahi Kiswahili

NGUVU ZA HOJA: Mabunge ya Kenya yatuzwa na chama cha CHAUKIDU kwa kustahi Kiswahili

NA PROF IRIBE MWANGI

ALHAMISI iliyopita niliandika kuhusu Kongamano la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) lililofanyika jijini Washington DC, Marekani.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na wajumbe wapatao mia mbili kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni lilifanyika katika Chuo Kikuu cha Havard chini ya uongozi wa Rais wake Prof Leonard Muaka.

Kulikuwa na warsha ya siku moja, mawasilisho ya wajumbe, vikao vya meza mduara na mawasilisho katika ukumbi mzima.

Prof Maulana Karenga, Prof Alamin Mazrui na Ustadh Abdilatif Abdala walitoa mada elekezi.

Balozi wa Tanzania Bi Elsi Kanza alitoa hotuba ya ufunguzi.

Siku ya Jumamosi kulikuwa na muda wa burudani ulioitwa ‘Usiku wa Mswahili’ ambapo washiriki waliburudishwa kwa vyakula, vinywaji na mavazi ya Waswahili pamoja na sarakasi.

Mgeni mashuhuri katika sherehe hii alikuwa Balozi Ann Wanjohi, Mkurugenzi wa Utamaduni na Diplomasia nchini Kenya na ambaye pia alitoa hotuba ya kufunga kongamano.

Katika sherehe hiyo kulitolewa tuzo kwa watu na mashirika ambayo yamechangia zaidi katika kukuza na kuendeleza Kiswahili.

Kati ya waliotuzwa ni Seneti na Bunge la Taifa la nchi ya Kenya.

Tuzo hizo zilikabidhiwa Balozi Wanjohi kwa niaba ya Bunge. Nilieleza sababu kuu ya kutuza Bunge kuwa kutafsiri Kanuni za Kudumu kwa Kiswahili.

Bunge la Tanzania pia lilituzwa kwa kutumia Kiswahili.

Shirika la UNESCO lilituzwa kwa kuteua Julai Saba kuwa siku ya Kiswahili Duniani. Tuzo yalo ilikabidhiwa Bi Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.

Prof Maulana Karenga alikabidhiwa tuzo ya ‘Mcheza Kwao’ kwa juhudi zake za kukisambaza Kiswahili hasa Marekani.

  • Tags

You can share this post!

Chipukizi hodari wa chesi apania kuvunja rekodi mashindano...

NDIVYO SIVYO: Matumizi yaliyozoeleka ya kauli ‘kwa...

T L