• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:26 PM
‘Nahisi upweke licha ya kuwa kwenye ndoa’

‘Nahisi upweke licha ya kuwa kwenye ndoa’

Na WINNIE A ONYANDO

MARIA na Steve wamekuwa kwenye ndoa miaka kumi sasa na tayari wamejaliwa watoto watatu.

Japo wawili hao huishi katika nyumba moja kama bibi na bwana, Maria anahisi upweke sana.

Mapenzi yaliyokuwa yakiongoza kati ya wawili hao yamegeuga kuwa usiku wa kiza kwa mrembo Maria.

“Japo sisi ni kitu kimoja, sihisi ananipenda tena. Nahisi nipo katika dunia yangu,” alilalamika Maria.

Madai kama haya hutokea mara nyingi katika ndoa. Utapata kuwa huenda mmoja kati ya wawili walioana anahisi kuwa mwenzake hampendi wala kumjali tena.

Haijalishi mmekuwa katika ndoa kwa muda mgani. Haya ni mambo yanayotokea kila kuchao.

‘Heri kuolewa au kumwoa mtu kwa misingi ya urafiki kuliko kuzingatia msingi wa kimapenzi.’

Mapenzi hupungua na hata kuisha ilhali urafiki hudumu.

Wakati mapenzi yanadidimia na yapo katika hatua za kufifia kabisa, basi urafiki kati ya wawili hao utayafufua mapenzi tena.

Maria anateta kuwa “Steve anashughulikia tu watoto ilhali mimi nimetengwa.”

Chochote kiletwacho katika nyumba yao ni ya watoto, hana raha kama mke kuwa huru kutumia chochote katika nyumba yake.

“Hajali hisia zangu, hanishirikishi katika uamuzi wake, ushauri wangu hauzingatiwi,” Maria anasema.

Ni hatari sana katika maisha ya ndoa ikiwa mmoja anahisi kuwa yupo mpweke. Matokeo yake huenda ikawagharimu wawili hao.

Upweke unawezamfanya mke au mume kutafuta ufariji nnje ya ndoa. Haya ndiyo chanzo cha faragha na ukosefu wa uaminifu katika ndoa.

Anapopata anayemjali, kumthamini, kumsifu na kumnunulia zawadi, basi mkondo unabadilika.

Anaanza kufuata ‘upepo’ na kuacha mbachao kwa msala upitao.

Wanawake ni viumbe wenye hisia sana, kila mwanaume ni sharti ajikakamue ili kumridhisha kihisia kadri iwezekanavyo.

Umpumbaze na zawadi, kumtengea muda, mpeleke matembezi na umwakikishie kila mara kuwa unampenda na kumthamini.

Sababu nyingine ya kuhisi upweke ingali upo katika ndoa ni matumizi mabaya ya simu. Huenda mmoja kati ya wawili hao anatumia simu kila mara na nafasi ya kuzungumza kama wanandoa kukosekana.

Kutoridhishana kimapenzi pia ni chanzo kingine cha kuhisi upweke katika ndoa. Huenda mke haridhishwi ipasavyo kimapenzi.

Ikiwa mume anajijali tu kihisia na kumsahau mkewe wakati wanashiriki mapenzi basi huenda hayo yakamfanya mke kuwa mpweke.

Wakati mwingine wanawake pia huwanyima waume zao haki zao. Matendo kama hayo huishia katika kuvunjika kwa ndoa hizo.

Upweke katika ndoa inawezasababisha kujiua, wasiwasi, kujistahi chini na hata ulevi na matumizi ya dawa za kulevya kwa mwathiriwa.

Ili kuondoa upweke katika ndoa, wawili hao wanaweza wakajadiliana, kutengeana muda ili wawe pamoja, kuenda likizoni pamoja, kufufua urafiki na mapenzi kati yao au hata kujadiliana na rafiki yako anayemthamini kuhusu suala hilo.

Usife na upweke.

  • Tags

You can share this post!

Dennis Waweru atangaza mchakato wa BBI kutamatishwa kabla...

Rais aenda mteja raia wakiumia