• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 10:55 AM
Eliud Kipchoge: Kuibuka mshindi wa Berlin Marathon mara tano ni ndoto niliyoweza kuota tu     

Eliud Kipchoge: Kuibuka mshindi wa Berlin Marathon mara tano ni ndoto niliyoweza kuota tu    

NA SAMMY WAWERU

BINGWA wa Dunia mbio za masafa marefu, Eliud Kipchoge ametaja ushindi wake wa tano katika Riadha za Berlin Marathon mnamo Jumapili, Septemba 24, 2023 kama ndoto ya ajabu.

Bw Kipchoge, 38, kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii amesema ushindi huo umemshtua na kumstaajabisha.

Aidha, ushindi wa mwaka huu umekuwa wa tano katika mbio za Berlin Marathon, hivyo basi kumuweka kwenye ramani ya dunia kuwa mwanariadha wa kwanza kutwaa taji hilo raundi tano.

“Kuwa wa kwanza kushinda Berlin Marathon mara tano, ni jambo ambalo niliweza kuota tu,” Kipchoge akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Chapisho hilo limeandamana na picha za mwanariadha huyo akishiriki mbio za Berlin Marathoni 2023, na pia akiinua bendera ya Kenya.

“Tuna historia nyingi pamoja ambapo siwezi kuelezea kwa maneno kutokana na ninavyohisi ninapotembea mitaani. Asanteni sana mashabiki wote walioungana nami leo,” akaelezea bingwa huyo.

Bw Kipchoge alitimka kwa muda wa saa 2, dakika 02 na sekunde 42.

Rais William Ruto ameongoza taifa kupongeza mwanariadha huyo ambaye amevunia Kenya sifa tele.

  • Tags

You can share this post!

FATAKI: Wakati umewadia tuongee kuhusu visa vya mauaji ya...

Ushauri nasaha kwa wanafunzi wa shule Nakuru kufuatia kifo...

T L