• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Mvinyo wa ‘white wine’ unavyotumiwa kudumisha urembo wa ngozi

Mvinyo wa ‘white wine’ unavyotumiwa kudumisha urembo wa ngozi

TUNAPOKARIBIA msimu wa sherehe, mojawapo ya aina ya vinywaji ambavyo vinatarajiwa kutumiwa na wengi ni mvinyo unaofahamika kama white wine.

Mvinyo wa white wine. Picha|maktaba

 

Lakini je, wajua kwamba, mbali na kutumika kama kinywaji, mvinyo huu pia ni kiungo muhimu katika shughuli za jikoni. Kando na hayo, ni kiungo muhimu katika masuala ya urembo ambapo unaweza kutumika kwa njia zifuatazo:

Huimarisha rangi ya ngozi: Changanya pamoja kijiko kimoja cha chai cha mvinyo na vikombe viwili vya maji. Unda mpira wa pamba kisha utumbukize mle ndani kisha upanguse uso wako msafi na usisuuze. Hii itachochea mzunguko wa damu katika sehemu hii, vile vile kupunguza vinyweleo.

Kutuliza ngozi: Ongeza milimeta 100 za mvinyo mweupe kwenye beseni yenye maji moto ya kuoga kisha ukae ndani kwa dakika 15. Hii itasaidia kulinda ngozi yako na kuimarisha usawa wa rangi yako.

Kusuuza nywele: Changanya mvinyo na maji na utumie mchanganyiko huo kusuuza nywele zako. Hii huondoa uchafu wa vumbi na masalio ya bidhaa zingine za nywele uliorundikana kwenye nywele zako na hivyo kuzifanya zing’ae.

Utulivu wa miyale ya jua: Changanya mvinyo na maji kisha utumbukize kitambaa mle ndani na utumie kupangusa maeneo yaliyochomeka kutokana na miyale ya jua. Hii husaidia kurejesha usawa wa kiwango cha pH kwenye ngozi yako.

Kitulizo cha uvimbe baada ya kunyoa nywele: Lowesha pamba kwenye siki ambayo haijachanganywa na maji, kisha upanguuse maeneo yaliyoathiriwa na uvimbe huu na uache kwa dakika tano kabla ya kusuuza kwa maji safi na kukausha. Hii itasaidia kutuliza ngozi inayowasha na kuifanya iwe nyepesi.

Kitulizo cha mba: Changanya viwangmweupe na maji kisha utumie mchanganyiko huu kusugua ngozi ya kichwa na nywele zako. Pia waweza changanya kijiko cha chai cha mvinyo huo kwenye sabuni maalum ya kuosha nywele (shampoo) yako ya kawaida na utumie kuosha nywele zako.

  • Tags

You can share this post!

Athari za El Nino: Barabara kuu ya Mombasa- Malindi...

Kaunti kuvuna Ripoti ya Kamati ya Mazungumzo ikipendekeza...

T L