• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Yaya aliyetunza watoto vizuri nchini Lebanon apongezwa kwa kuizolea Kenya sifa nzuri

Yaya aliyetunza watoto vizuri nchini Lebanon apongezwa kwa kuizolea Kenya sifa nzuri

NA FRIDAH OKACHI

YAYA Mkenya Rozah Rozalina Samson almaarufu ‘Rosie’, anayefanya kazi nchini Lebanon, amekuwa mtu maarufu mtandaoni baada ya kuacha mashabiki wa mitandao na hisia kutokana na tukio la kuhuzunisha la kuaga mwajiri wake na watoto anaowalea.

Kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Maria.Cataleya ambayo kufikia sasa imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, katika uwanja wa ndege wa Lebanon, tukio la hisia lilijitokeza wakati familia ya mwajiri wake huyo ilijitahidi kumuaga yaya wao mpendwa.

Yaya huyo alikuwa akiwalea watoto wanne na alikuwa akirejea nchini Kenya ili kuanza likizo.

Video hiyo imesisimua na kuonyesha watoto wa mwajiri wake–ambao ni pacha–wakilia kwa uchungu na kumfuata yaya huyo kwa upendo huku machozi yakimtiririka pia.

Wazazi wa watoto hao walipata wakati mgumu kuwanyamazisha na kuwatenganisha na Rosie.

Wakati huo, mama ya watoto hao alisiskika kwenye video hiyo akiwahimiza kuwa yaya huyo atarejea.

“Atakuja tena, naomba mumuage ili aanze safari,” alisikika akisema.

Katika video hiyo iliyochapishwa na mwajiri wa Rosie, alipakia na ujumbe wa kumshukuru yaya huyo.

“Asante, Rosie, kwa kulea wanangu kama wako,” alichapisha.

Kabla ya kuondoka kwake Rosie, familia hiyo ilikuwa imemfanyia karamu ya siku ya kuzaliwa na kumtambua si mfanyikazi tuu bali mmoja wa familia yao.

Video hiyo imevutia watu wengi nchini Kenya ambao warifurika kwenye mitandao ya kijamii na ujumbe wa kumuunga mkono kwa wema wa Rosie kwa watoto wa mwajiri wake.

Miongoni mwa walioguswa na video hiyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Expedition Maasai Safaris, Pancras Karema yupo kwenye harakati ya kumtafuta Rosie ili kumzawadi kwa kazi yake.

Katika taarifa yake Bw Karema alisema kutuzwa kwake ni kutokana na kuonyeshana kuwa wakenya wanatambuliwa kwa bidii yao.

“Tunatambua na kumtuza Rosie kwa kuonyesha ulimwengu kile wafanyikaza wa Kenya wanafanya. Tafadhali nisaidie kumpata. Tungepanda kumpa zawadi ya likizo kama ishara ya shukrani zetu!” alisema Bw Karema.

Katika chapisho lingine, Kampuni ya Expedition Maasai Safaris ilisisistiza Rosie alikuwa na moyo wa dhahabu na kuelezea hamu ya kampuni hiyo kumsherekea kwa likizo ya bure nchini Kenya.

“Huyu mwanamke wa Kenya aliye na moyo wa dhahabu anastahili kutambuliwa na kutuzwa kwa kuonyesha ulimwengu kile ambacho wafanyikazi wa Kenya jinsi wameumbwa-Kujitolea, azma na unyenyekevu. Unaona hata watoto hawataki aondoke. Tunataka kumsherekea na likizo ya bure,” aliendelea.

  • Tags

You can share this post!

NSC yatahadharisha Wakenya kuhusu aina 30 za uhalifu msimu...

Vijana, akina mama wapokezwa ujuzi kukabiliana na itikadi...

T L