• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Polo na kahaba wakwamiliana lojing’i Othaya

Polo na kahaba wakwamiliana lojing’i Othaya

NA MWANGI MUIRURI

KIZAAZAA kilizuka katika danguro moja la mahaba Mjini Othaya, baada ya mwanamume na mwanamke kukwamiliana baada ya kulala usiku kucha wakishiriki mahaba.

Kwa mujibu wa mdokezi wetu katika ng’weni hilo lililoko katikati mwa mji huo wa kuzaliwa kwa Rais wa tatu nchini Mwai Kibaki, wawili hao walijipata wamenaswa na mtego wa ushirikina kutoka kwa mume wa mwanamke huyo.

“Ilibainika kwamba mwanamke huyo alikuwa amekwepa ndoa yake na kuingia mtaani kuwa kahaba ili kusaka pesa. Lakini bwanake bila kumuarifu, alitafuta huduma za ushirikina na kufunga mzinga wake wa asali,” akasema mdokezi wetu.

Bila kujua kuhusu mtego huo, mwanamke huyo wa miaka 42 alipata mteja wa kulala naye mwendo wa saa tano usiku wa Desemba 1, 2023 kwa dili ya Sh1, 000.

“Hatujui wawili hao walikwamiliana saa ngapi lakini asubuhi ya saa tatu makahaba wengine katika danguro hilo walipata sauti za kulalama zikitoka kutoka kwa chumba cha mwenzao na taharuki ikatanda, ikidhaniwa mauti yalikuwa yamefika katika danguro hilo,” akaongeza.

Ilibidi bawabu aitwe na mlango kuvunjwa, ndipo wawili hao walipatikana wakijaribu kujinasua.

Wakionekana kulemewa na machovu ya kujiokoa, walikuwa tayari wameanguka kutoka kwa kitanda huku wakisubiri usaidizi wakiwa sakafuni.

Lalama zilitawala chumba walimokuwa.

“Kuna mwanamke kahaba ambaye alikuwa anaelewa mambo haya na ndiye alitwambia tuwaitishe wawili hao nambari za bwana na bibi zao na ambapo mwanamume alisema hana bibi,” bawabu wa maeneo hayo akatuarifu.

Mama alipeana namba ya simu ya bwanake na ambaye baada ya kupigiwa, alifika mwendo wa saa nne na nusu akiandamana na mwanamke aliyetambulishwa kama mganga.

“Mganga aliingia katika chumba hicho na baada ya kukagua kazi aliyokuwa ameitiwa, akadai malipo ya Sh3, 000 huku naye mwanamume mwenye bibi akidai fidia ya Sh10, 000 ya kuchafuliwa mazingira ya mzinga wake,” akasema bawabu.

Kwa bahati njema, mwanamume aliyekuwa amekwama ndani ya mwanamke huyo alikuwa na pesa kwenye simu na akatuma gharama yote ya Sh13, 000.

Alizabwa kofi moja tu la makalio na mganga huyo na akakwamka.

“Polo alipokwamka alivaa nguo zake kwa haraka na akaondoka eneo hilo akionekana kushtuka si haba, mwanamume akiondoka pamoja na mganga wake na kumuacha bibi yake nyuma. Bibi aliamka na akavaa nguo zake na kuondoka bila kuelezea alikuwa aelekee wapi huku sisi tukibakia kuduwazwa na nguvu hizo za ushirikina zilizogeuza ngoma ya wawili kuwa balaa ya kukwamiliana,” akasema bawabu mdokezi.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Vijana waonywa dhidi ya ngono bila kinga

Samidoh ampa mfuasi wake tonge la majibu

T L