• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Saba Saba: Raila Odinga ataka Chebukati asukumwe jela

Saba Saba: Raila Odinga ataka Chebukati asukumwe jela

NA SAMMY WAWERU

KINARA wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesisitiza mageuzi kufanyika katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), akitetea msimamo wake kuwa utaletea taifa uwazi wakati wa chaguzi.

Akihutubu Ijumaa, Julai 7, 2023 katika maandamano ya muungano huo wa upinzani Nairobi, Bw Odinga alisema mabadiliko kwenye tume yataanza kutafanyika endapo aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati atasukumwa jela.

Maandamano ya Azimio yamelingana na siku ya Saba Saba, inayofanyika Julai 7 kila mwkaa kama kumbukumbu ya oparesheni kutetea uhuru wa demokrasia Kenya na utawala wa vyama vingi iliyofanyika mnamo Julai 7, 1991.

Bw Odinga alikuwa miongoni mwa viongozi na wanasiasa walioshiriki.

Kiongozi huyo wa upinzani alitoa kauli ya mageuzi katika IEBC, akidai Bw Chebukati “alicheza na Wakenya kwa kuwanyima haki yao Kikataba kupata kiongozi waliyedhania angeingia Ikulu”.

“Kwanza tunataka Wafula Chebukati aingie ndani (akimaanisha jela),” Bw Odinga akasisitiza.

Katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2023 Raila Odinga aliwania urais kupitia mrengo wa Azimio, akimenyana na Rais wa sasa William Ruto aliyembwaga.

Kesi yake kutaka matokeo ya urais yafutiliwe mbali hata hivyo iliangushwa na Mahakama ya Juu zaidi.

“Tunataka mabadiliko katika IEBC na lazima Azimio ihusishwe, ikiwemo makamishna waliofutwa kazi warejeshwe,” Bw Odinga akasisitiza.

Makamishna waliotimuliwa ofisini na wengine kujiuzulu kufuatia presha ya matokeo ya urais Agosti 9, ni pamoja na Juliana Cherera (naibu mwenyekiti IEBC), Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya.

Mgawanyiko ulishuhudiwa katika IEBC, nne hao wakijitenga na matoeko ya urais.

  • Tags

You can share this post!

SABA SABA: Yanayojiri kutoka kona zote za nchi

Polisi wakamata waandamanaji 3 Banda Street, wawakanyaga...

T L