• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Silafrica: Yatengeneza bidhaa za plastiki na kusaidia katika uhifadhi wa mazingira

Silafrica: Yatengeneza bidhaa za plastiki na kusaidia katika uhifadhi wa mazingira

NA MAGDALENE WANJA

KWA muda wa zaidi ya miongo minne, kampuni ya Silafrica imekuwa ikiongoza katika utengenezaji wa mikebe ya kupakia iliyotengenezwa kwa plastiki.

Kampuni hii hutengenezea kampuni mbalimbali nchini ambazo ziko katika biashara ya bidhaa kama vile vyakula, vinywaji, mafuta, siagi, gururu na tangi za plastiki za kufadhia maji.

Kampuni ya Silafrica iko katika sekta ya utengenezaji wa mikebe ya kupakia iliyotengenezwa kwa plastiki na inatengeneza pia matangi ya maji. PICHA | MAGDALENE WANJA

Mkurugenzi mkuu Bw Akshay Shah anasema kuwa alipozaliwa, familia yake ilikuwa tayari kwenye biashara mbalimbali ya sekta ya viwanda nchini Tanzania, jambo ambalo lilisaidia katika kukua kwa biashara hiyo nchini Kenya.

Haja kuu ya kampuni hiyo kuingia katika baadhi ya nchi nyingine barani Afrika ilipelekea kuanzisha kwa viwanda katika nchi za Ethiopia, Nigeria na Uganda.

Kampuni ya Silafrica iko katika sekta ya utengenezaji wa mikebe ya kupakia iliyotengenezwa kwa plastiki na inatengeneza pia matangi ya maji. PICHA | MAGDALENE WANJA

Nchini Nigeria, kampuni hiyo ilifanya kazi na baadhi ya kampuni ikiwemo ile ya Coca-Cola, lakini ililazimika kufunga kutokana na mazingira mabaya ya biashara.

Nchini Uganda, biashara haikufanya vyema pia kutokana na kile mwanzilishi anasema kulikuwa ni msimu uliokuwa wa kisiasa.

“Kampuni ya kwanza ilikuwa nchini Tanzania, na imechangia katika kukua kwa biashara katika nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Milki za Kiarabu (UAE),” akasema Shah.

Kampuni ya Silafrica iko kipaumbale kusaidia biashara ndogo zinazojulikana kama SMEs ili kufikia malengo yao ya kukua kibiashara.

Mfanyakazi wa kampuni ya Silafrica akitengeneza bidhaa mojawapo ya plastiki. PICHA | MAGDALENE WANJA

Kufikia sasa, zaidi ya kampuni 80 humu nchini zimefaidika kutokana na mpango huu.

“Kampuni ya Silafrica ilianza kama SME na hivyo tunajivunia sana katika kusaidia biashara ndogondogo,” anasema.

Matumizi ya vyombo vya plastiki mara zaidi ya moja husaidia katika upungufu wa uchafuzi wa mazingira.

Kampuni hiyo huzichaka upya plastiki ili kutengeneza kreti za kubebea bidhaa za kuuzwa katika mataifa ya nje.

Mojawapo ya kampuni ambazo hutumia kreti hizo ni pamoja na shirika la Avocado Society of Kena ambalo huuza matunda hayo katika mataifa mengine.

  • Tags

You can share this post!

Gavana Nassir aonya mawaziri wake dhidi ya uzembe

Jinsi ndoa 55 zilivyonoga kwa hafla ya pamoja

T L