• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
TALANTA YANGU: Dogo mkali wa kubofya piano

TALANTA YANGU: Dogo mkali wa kubofya piano

MAFUNZO ya namna ya kucheza piano huendeshwa hatua kwa hatua kwa sababu kila kibonye cha kibodi hutoa sauti tofauti.

Kwa mwanafunzi Athur Israel Njoroge, kucheza piano ni mojawapo ya juhudi zake katika safari ya kuwa kasisi siku za baadaye.

Njoroge ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 katika Shule ya Msingi ya Children in Freedom Lanet Kaunti ya Nakuru, anasema alianza kucheza piano akiwa na miaka minane.

“Hii ni baada ya kubaini kuwa si watu wengi walikuwa na ujuzi wa kucheza piano,”akasema, akiogeza kuwa mbinu za mkono zinahitajika wakati wa kujifunza namna ya kucheza piano.

Pili, anasema kuwa stadi ya kucheza piano ni rahisi mradi mwenye mapenzi afanye mazoezi ya mara kwa mara, ajiwekee malengo, bidii na nidhamu.

Aidha, afuate maelekezo kutoka kwa walimu wake kwani huu ni mchezo ambao unahitaji mpigaji kuwa na subira nyingi kabla ya kujiboresha na kuwa gwiji, bila kusahau kuwa ni rahisi kukata tamaa.

Njoroge anasema kwamba yeye hupiga piano kwenye kanisa linalopatikana katika barabara ya Kenyatta Avenue jijini Nakuru linalofahamika kama Chosen Generation Church.

Ili kuhakikisha anaendeleza kipaji chake, vilevile yeye huwatumbuiza wanafunzi wenzake shuleni wakati wa vipindi vya muziki, wakati wa mapumziko ama siku za wazazi.

Kwa mujibu wa Njoroge, amekuwa akitumia mtandao wa kijamii kujifunza namna ya kutengeneza midundo mipya na vilevile husikia aina nyingi ya nyimbo nyingi yazo zikiwa ni zile za injili.

Anasema kuwa tangu aanze kucheza piano amebaini kuwa wanafunzi wenzake wanapenda sana kusikiliza nyimbo na ndio maana kila siku amejitwika jukumu la kuhakikisha analinda ala hii ya muziki, popote aipatapo.

Anawashauri wanafunzi wenzake wasijue tu jinsi ala ya muziki inavyofahamika bali pia wajizatiti kufahamu namna ya kuicheza, akiamini kuwa hii ndiyo njia muafaka ya kufaidi ujifunzaji wa ala za muziki.

Aidha, anasema kwamba njia sahihi ya kujifunza uchezaji wa ala za muziki utategemea mambo mengi kama vile ukaribu na mkufunzi ambaye anatoa mafunzo ya kucheza ala husika ya muziki.

  • Tags

You can share this post!

Papa Francis akamilisha ziara yake Sudan Kusini

PAUKWA: Mchelea mwana kulia hulia yeye mwenyewe

T L