• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Tiba rahisi za nyumbani kwa mzio wa ngozi na vipele

Tiba rahisi za nyumbani kwa mzio wa ngozi na vipele

NA MARGARET MAINA

[email protected]

UNAWEZA kuona sehemu nyekundu iliyovimba ambayo inauma kwenye ngozi yako na kujiuliza ni nini.

Inaweza kuwa upele. Upele unaweza kuwa kiashiria cha matatizo kadhaa ya kiafya. Unaweza kutokea kutokana na kuwasha (dutu inayosababisha mwasho) au mzio.

Kwa vile upele unaweza kusababishwa na vitu nyingi, ni muhimu kubaini sababu hasa ni nini ndipo upate matibabu yanayofaa.

Unaweza kuwa na mzio wa vitu fulani, na vitu hivi vinapogusa ngozi yako vinaweza kusababisha kutokea kwa upele. Kwa hivyo, upele unaweza kutokea kwa sababu ya mzio wa ngozi pia. Ingawa upele unaweza kuwa mbaya na unasababisha uchungu, hauwezi kuambukiza. Yaani hauwezi kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Hata hivyo, ili kulainisha ngozi yako, kuna njia mbalimbali za nyumbani za kukabili upele ambazo unaweza kuziona zinafaa.

Baadhi ya vitu vilivyo katika mazingira kama vile chavua, ukungu, au mimea na wanyama vinaweza kusababisha athari ya mzio kwenye ngozi, haswa wakati wa kiangazi au masika. Mimea michache na nyasi zinaweza kusababisha upele wa ngozi kwa sababu ya mzio.

Jasho na joto huweza kusababisha mzio. Kwa kutokwa na jasho kupindukia, unaweza kukabiliwa na ukurutu unaozidi kuwa mbaya.

Wakati ngozi inapogusana na dutu inayosababisha mzio, inatahadharisha mfumo wa kinga, na kusababisha upele kwenye ngozi.

Dalili za mzio wa ngozi na vipele:

Itakuwa nyekundu kwa rangi, kuwasha na inaweza kuchoma au kuuma

Inaweza kuhusishwa na kuwaka au kupanuka kwa ngozi kwenye upele

Inaweza kuwa chungu

Inaweza kuwa na kuvimba, kutokwa na damu au inaweza kuwa na uvimbe.

Tiba za nyumbani zinazopendekezwa

Mzio wa ngozi na vipele ni jambo la kawaida tunapokutana na vizio kadhaa wakati wa shughuli zetu za kila siku. Matibabu ya vipele hivi yanaweza kuwa ya aina mbalimbali, kama itakavyopendekezwa na daktari wako.

Huenda ikachukua muda kwa upele kutoweka hata baada ya kuanza matibabu.

Hata hivyo, kuna tiba za nyumbani za upele ambazo unaweza kujaribu ikiwa unatafuta tiba asilia za upele na mzio wa ngozi.

Majani ya Chamomile, jeli ya mshubiri, shayiri na mbegu za kitani ni baadhi ya njia asili za kutuliza na kupunguza vipele nyumbani.

  • Tags

You can share this post!

Shujaa yatiwa kundi la kifo Dubai Sevens

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu bambam na mwanamitindo stadi

T L