• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Tiba za nyumbani kwa wenye maumivu ya meno

Tiba za nyumbani kwa wenye maumivu ya meno

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MAUMIVU ya jino hutokea wakati neva ndani ya jino zinapowasha au kuna maambukizi ya bakteria wanaosababisha jipu karibu na jino.

Ikiwa sababu zinazopelekea maumivu ya jino ni kidogo na zinaweza kutibika nyumbani, huenda usihitaji kutembelea daktari wa meno.

Kwa upande mwingine, maumivu ya meno yanayosababishwa na kuvimba kwa ufizi na kuoza kwa meno ambayo hayatapungua kwa tiba za nyumbani yatakulazimu utafute ushauri wa daktari.

Maumivu ya meno hutokea kutokana na usafi duni wa meno au yanaweza kuchochewa na mambo mengine mbalimbali.

Wakati mwingine maumivu ya jino hayawezi kuvumilika na yanaweza kukufanya ukae macho usiku kucha, tena kwa kutaabika.

Kwa hiyo, kuna tiba chache za nyumbani ambazo unaweza kujaribu.

Karafuu

Karafuu ni kiungo maarufu cha chakula. Inaweza kutumika kupambana na kuoza kwa meno na harufu mbaya ya kinywa.

Karafuu inaweza kuwa na vipengele ambavyo hupunguza maumivu na kupunguza kuvimba. Ili kutengeneza unga wa karafuu, chukua bakuli dogo la kuchanganya na uponde karafuu kwa kutumia matone machache ya maji ili kuandaa unga mzito. Kisha, weka hii kwa meno yaliyoathirika.

Mbegu ya parachichi

Mbegu ya parachichi ina antifungal muhimu dhidi ya fangasi na kuvu mbalimbali. Mbegu za parachichi zinaweza kuwa na manufaa kwa wenye kuhisi maumivu ya meno. Ili kutumia mbegu za parachichi, ziponde na kuzichemsha kwenye maji.Tumia maji yanayopatikana kwa kusuuza kinywa. Kufanya hivi kunaweza kukusaidia kupunguza maumivu na vidonda mdomoni.

Kitunguu saumu

Kitunguu saumu ni kimojawapo cha viungo vinavyopendwa sana. Kimekuwa kikitumika kama mmea wa dawa kwa karne nyingi. Sifa hizi za kitunguu saumu zinaweza kuwa muhimu kwa ajili ya udhibiti wa shida ya meno.

Kitunguu saumu. PICHA | MARGARET MAINA

Vitunguu vinaweza kusababisha hisia inayowaka hivyo mtumiaji anafaa kuepuka kutumia kupita kiasi na pengine unaweza kunywa maziwa mengi ili kuondokana na hisia inayowaka au ukatumia asali ili kuzuia harufu ya vitunguu.

Papai

Mbegu ya papai na majimaji meupe yanaweza kuwa na manufaa dhidi ya maumivu ya jino. Papai huwa na uwezo wa kuzuia ukuaji wa bakteria kinywani. Mbegu za papai zinaweza kuwa na antifungal inayosaidia dhidi ya maumivu ya meno.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Kunaendaje Rais na ni wewe uliahidi kuwa...

Umuhimu wa kula vitamini mara kwa mara

T L