• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:55 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Kunaendaje Rais na ni wewe uliahidi kuwa fedha za Hazina ya Hasla hazingetozwa riba yoyote?

TUSIJE TUKASAHAU: Kunaendaje Rais na ni wewe uliahidi kuwa fedha za Hazina ya Hasla hazingetozwa riba yoyote?

MNAMO Jumamosi wiki jana, Rais William Ruto aliahidi kuwa serikali itaanzisha Hazina ya Hasla mwezi Desemba 2022 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo nchini.

Akiongea katika kaunti ya Kirinyaga alipoongoza shughuli ya uzinduzi wa Bwawa la Thiba, Dkt Ruto alisema mkopo huo utatozwa riba “nafuu” ya chini ya asilimia 10 ili kuhakikisha idadi kubwa ya wafanyabiashara wanafaidi.

Alikariiri kauli hiyo mnamo Jumapili mjini Kericho aliposema hivi: “Hakuna pesa za serikali zitatolewa bure.”

“Ukikopa pesa za serikali ili kupiga jeki biashara zako sharti urudishe kwa riba ndogo isiyozidi asilimia 10,” akaongea katika uwanja wa michezo wa Kericho Green wakati wa hafla ya maombi ya kutoa shukrani.

Lakini Rais asije akasahau kuwa katika misururu ya kampeni ya kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, Rais aliahidi kuwa fedha za Hazina ya Hasla hazingetozwa riba yoyote.

You can share this post!

Faida za mbegu za katani

Tiba za nyumbani kwa wenye maumivu ya meno

T L