• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
ULIMBWENDE: Njia mbalimbali za kuipa ngozi yako mng’ao wa kipekee

ULIMBWENDE: Njia mbalimbali za kuipa ngozi yako mng’ao wa kipekee

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WATU wengi hujivunia kuwa na ngozi yenye mwonekano wa kipekee.

Watu huwa wanatumia kiasi fulani cha kipato chao kwa ajili ya utunzaji wa ngozi zao.

Hivyo ni vyema ukawa na ufahamu sahihi wa jinsi gani ya kutunza ngozi yako ili isizeeke mapema.

Hizi ni baadhi ya njia za kutumia kuitunza ngozi yako.

Hakikisha unaepuka mionzi ya jua kwa kadri inavyowezekana

Hii ni njia muhimu sana ya kuitunza ngozi yako. Si lazima uwe na pesa nyingi kutimiza hili; ni wewe tu kubadilisha mtindo wa maisha. Ifahamike mtu ambaye hakuepuka mionzi ya jua kwa miaka mingi katika maisha yake anaweza akapata saratani ya ngozi. Pia ngozi hujikunja mapema, huwa na madoa meusi na kukabiliwa na matatizo mengine ya ngozi.

Ni vyema ukatumia vipodozi vinavyozuia mionzi ya jua wakati wa mchana.

Vaa mavazi yanayofunika sehemu kubwa ya mwili. Pia ni muhimu kuvaa kofia na upende kukaa kwenye kivuli.

Usivute sigara

Uvutaji wa sigara unafanya ngozi yako ijikunje na kuzeeka mapema. Hii ni kutokana na kwamba uvutaji wa sigara unafanya mirija iliyo midogo katika sehemu ya nje ya ngozi kuwa na uwazi mdogo na hivyo kupelekea hewa ya oksijeni na virutubisho muhimu kutotosha kwa ajili ya afya ya ngozi. Uvutaji wa sigara huharibu ‘elastin’ na ‘collagen’ ambazo kwa pamoja hufanya ngozi kuwa imara.

Hakikisha unakula matunda na mboga za majani kila mara

Matunda yenye vitamini C ni muhimu sana kwani vitamini C huzuia ngozi kuzeeka mapema. Hii hutokana na uwezo wake wa kuzuia seli za ngozi kuharibiwa na sumu ambazo ni ‘oxidants’. Haya matunda ni kama machungwa na limau.

Pia chakula chenye vitamini E ni muhimu katika ustawi wa ngozi. Chakula hiki ni kama karoti.

Mboga za majani ni muhimu sana katika ustawi mzuri wa ngozi.

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha

Jinsi unavyopata usingizi wa kutosha ndivyo hata ngozi hujiweka vizuri na hivyo kuwa na mwonekano mzuri.

Usafi binafsi wa mwili

Ni vyema kuisafisha ngozi yako mara mbili kwa siku wakati wa asubuhi na usiku na wakati wowote ikiwa umetokwa na jasho jingi. Chunga usitumie sabuni kali ila tumia aina za kawaida za kuogea haswa kwa watu wenye ngozi yenye mafuta. Pia hakikisha unatoa vipodozi vyote kabla ya kuingia kitandani kulala. Hakikisha kitanda chako na mito ni safi.

Kunywa maji ya kutosha

Ngozi inahitaji maji.

Fanya mazoezi

Mazoezi yanafanya mzunguko wa damu uwe mzuri na hivyo kufanya ngozi kuwa na ustawi mzuri.

Tumia vipodozi vizuri vinavyoendana na ngozi yako

Kuna baadhi ya vipodozi ambavyo ni vikali sana na ukivutumia vinakupatia matokeo unayoyataka kwa muda mfupi lakini kiukweli ni hatari sana. Madhara yake ni kama ngozi kuwa nyembamba sana isiyoweza kuulinda mwili vizuri, ngozi kuzeeka mapema na saratani ya ngozi. Hivyo, chagua vipodozi vinavyooendana na ngozi yako. Hii ina maana kwamba kama ngozi yako ni kavu, unafaa kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi hiyo na kama ina mafuta tumia vipodozi kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

  • Tags

You can share this post!

Kiunjuri, Mbunge waagizwa kufika mbele ya IEBC

ULIMBWENDE: Tumia maziwa kulainisha ngozi yako

T L