• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Umuhimu wa mafuta ya cod liver

Umuhimu wa mafuta ya cod liver

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MAFUTA ya cod liver ni chanzo bora cha vitamini na asidi ya mafuta.

Mafuta haya hupatikana kutoka kwa samaki ambapo ini hutumiwa kutoa mafuta yenyewe.

Uwepo wa vitamini na asidi muhimu katika mafuta ya cod liver unaweza kuwa wa manufaa kwa wanadamu kwa sababu mbalimbali.

Kupunguza lehemu

Ulaji wa mara kwa mara wa asidi ya Omega-3 husaidia kupunguza uundaji wa lehemu mbaya katika mwili wa binadamu. Mafuta ya cod liver ni chanzo kikubwa cha vitamini na asidi ya mafuta ya Omega-3.

Matumizi ya mafuta ya cod liver kwa vidonda vya tumbo

Uwepo wa vitamini na asidi muhimu ya mafuta husaidia katika shughuli za antioxidants katika mwili.

Mafuta haya yanaweza kulinda dhidi ya vidonda vya tumbo ambavyo vinaweza kupunguza utolewaji wa asidi na kulinda utando wa ndani wa tumbo.

Uwezekano wa matumizi ya mafuta ya ini ya cod kwa uponyaji wa jeraha

Vitamini A iliyopo katika mafuta haya inaweza kuongeza kasi ya kuundwa kwa seli za ngozi kwenye jeraha.

Mafuta ya cod liver kwa ngozi

Mafuta haya yanaweza kuwa na asidi ya mafuta kama vile asidi ya mafuta ya Omega-3, ambayo inaweza kufanya ngozi kuwa na maji na kupunguza ukavu wa ngozi. Asidi za mafuta zinaweza kuleta mng’ao wa ngozi na pia kuzuia kuwasha. Ikiwa una masuala yoyote yanayohusiana na ngozi, lazima uwasiliane na daktari wako kabla ya kutumia mafuta ya cod liver kwa ngozi.

Matumizi ya mafuta ya cod liver kwa ugonjwa wa yabisi

Ugonjwa wa yabisi unahusishwa na uvimbe na maumivu katika viungo. Utumiaji wa mara kwa mara wa mafuta ya cod liver unaweza kupunguza ugumu wa viungo asubuhi na maumivu ya viungo. Hata hivyo, ikiwa unapata maumivu mengi, lazima uwasiliane na daktari wako.

  • Tags

You can share this post!

Tiba za nyumbani za kukusaida endapo umechomwa na jua

Ruto aomba muda wa kutimiza ahadi

T L