• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Unapoliosha gari, hakikisha hutumii maji ya chumvi

Unapoliosha gari, hakikisha hutumii maji ya chumvi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WATU wengi wamekuwa hawatumii vifaa sahihi wakati wanaosha magari yao na hata wale wanaomiliki sehemu za kuoshea magari baadhi yao nao wamekuwa hawana vifaa sahihi.

Wengi wakidhani tu kwamba kuwa na sabuni, maji na mashine ya kutolea maji kwa spidi ndio nyenzo muhimu za biashara ya kuosha magari.

Kumbe watu wenyewe ndio wanaharibu magari yao na hata ya wateja wao.

Epuka maji ya chumvi

Wenye magari wengi hawafahamu iwapo maji yanayotumika kuoshea magari yao ni ya chumvi au la.

Usitumie maji ya chumvi katika kuosha gari lako kwa sababu maji ya chumvi hukwaruza na kuondoa rangi ya gari. Pia maji ya chumvi husababisha gari lako kushika kutu pamoja na kusababisha vioo vya gari kuwa na vidotidoti. Usipende kutumia maji ya chumvi katika kuosha gari lako.

Usitumie aina ya sabuni ambayo sio sahihi kwa ajili ya kuoshea magari

Baadhi ya watu wanadhani sabuni ni sabuni tu na hakuna tofauti. Fahamu kwamba kila sabuni imetengenezwa kwa matumizi yake. Kwa mfano, kuna sabuni iliyotengenezwa kwa ajili ya kusafisha choo na huwezi kuitumia kusafishia vyombo kwa sababu malighafi yaliyotumika kutengeneza sabuni hiyo yalikusudiwa kwa ajili ya chooni.

Unapotumia sabuni ambayo sio sahihi katika kuoshea gari basi fahamu kuwa unaelekea kuharibu rangi ya gari lako na kusababisha kutu kwenye gari. Usitumie sabuni ya kuoshea vyombo wala sabuni ya kufulia – ya unga – katika kuoshea gari lako. Badala yake tafuta sabuni sahihi kwa ajili ya kuoshea magari.

Osha gari lako likiwa kivulini

Ni muhimu sana kuosha magari yetu kwenye sehemu iliyotengenezwa kuzuia miale ya jua kwa sababu unapoosha gari lako kwenye jua hukaushwa likiwa lingali na maji na sabuni. Likikauka upesi kabla ya uoshaji kukamilika, gari hubaki na michirizi ambayo inakuwa migumu kutoka wakati wa kufuta gari baada ya kuosha.

Safisha ndani ya gari lako

Kusafisha ndani ya gari huchukua muda mfupi. Unapaswa kuondoa na kutupa vitu vyote vilivyomo ndani ya gari ambavyo havina kazi na wala havitumiki tena ili lionekane nadhifu na lenye mvuto ndani.

Tumia vifutio laini katika kufuta sehemu kama dashboard, milango, ndani ya mifuko ya milango, katikati ya gari kwenye viti na sehemu nyingine kwa ajili ya kuondoa vumbi na uchafu.

Lakini pia unashauriwa kulipulizia air freshener ili kufanya gari lako kuwa na harufu ya kuvutia.

You can share this post!

Ubabe wa Mvurya, Joho kuibuka upya

Mzee aliyesaidia Kenyatta gerezani ataka atambuliwe

T L