• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
USHAURI NASAHA: Thamini mazoezi ya kimwili hata sasa ufanyapo mtihani

USHAURI NASAHA: Thamini mazoezi ya kimwili hata sasa ufanyapo mtihani

NA HENRY MOKUA

KILA shule inapojitahidi kuimarisha matokeo ya wanafunzi wayo masomoni hasa wakati huu wa mitihani ya kitaifa, nyingi katika shule hizi zimepunguza muda wa mazoezi ya kimwili ili kuongeza muda wa kudurusu.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani, katika Taasisi ya Uuguzi, umeonesha kwamba hatua hii haina maono.

Kwa mujibu wa utafiti, mazoezi huimarisha kwa kiasi kikubwa uwezo wa kiakili wa wanafunzi, matokeo yao masomoni na afya zao.

Wanafunzi wanaofanya mazoezi ya kimwili hupunguza kiwango cha mafuta miilini, kuzidisha nguvu za misuli yao na kuimarisha afya za akili zao.

Wanajopo waliofanya utafiti huu wanaeleza kwamba watoto wafanyao mazoezi zaidi hudumisha makini zaidi, hutekeleza majukumu mepesi kwa haraka, huwa na kumbukizi bora na hutatua migogoro kwa urahisi kuliko wenzao wasiofanya mazoezi.

Aidha, huwa wanafanya vyema katika mijarabu iliyosawazishwa.

Utafiti huu unapendekeza kwamba wanafunzi wote wapate angalau dakika sitini za kufanya mazoezi ya kimwili kwa wastani, sawa na kutembea haraka.

Asilimia inayotumia muda huu kwa mazoezi ni ndogo kuliko inayotumia kwa masomo ya ziada.

Njia mwafaka ya kuongeza muda huu ni kuongeza vipindi vya mazoezi ya mwili kwenye ratiba zetu, muda wa breki, na kuhimiza spoti baada ya vipindi vya siku. Kutembea wakati wa kuenda na kurejea kutoka shuleni kunaweza kufaa pia kwa mwanafunzi wa kutwa.

Mazoezi ya kimwili yanapaswa kuthaminiwa mno kwani ni kitovu cha kufanikiwa masomoni; si mbadala unaoweza kupuuzwa.

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Jinsi Morocco walivyotoa miamba...

Mbunge amshambulia Winnie Odinga

T L