• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 10:55 AM
Wakili Ndegwa Njiru: Polisi Watamu walikuwa wanasubiri amri kutoka juu kumwasilisha bloga Pauline Njoroge kortini

Wakili Ndegwa Njiru: Polisi Watamu walikuwa wanasubiri amri kutoka juu kumwasilisha bloga Pauline Njoroge kortini

NA SAMMY WAWERU

NAIBU mratibu chama cha Jubilee, Pauline Njoroge amewasilishwa Jumatatu, Julai 24, 2023 katika Mahakama Malindi ambapo anaandamwa na tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya.

Bi Pauline, ambaye pia ni bloga wa Azimio, alikamatwa mnamo Ijumaa, Julai 21 na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Watamu, Kilifi.

Alitiwa nguvuni pamoja na washukiwa wengine wawili.

Bi Pauline, Jane Mwangi Nduta na Emanze Jilani walikamatwa na makachero wa DCI gari walilokuwa wakitumia liliposimamishwa katika barabara ya Watamu kuelekea Jakaranda.

Kulingana na Wakili wa Mwanablogu huyo, Ndegwa Njiru kabla kufikishwa kortini askari walidai wamepokea masharti makali wakisema walitakiwa kusubiri amri kutoka ‘juu’ ili kuruhusiwa kumfungulia mashtaka.

“Tunaelewa kituo cha Polisi cha Watamu kilikuwa na watu wengine waliokamatwa na ambao walifikishwa mahakamani.

“Wateja wetu wangali kwenye seli. OCS hawezi kutoa uamuzi kwa sababu hajajua ni nani anayepaswa kutoa amri kuwapeleka kortini,” Bw Njiru aliambia wanahabari.

Wakili huyo aliyeandamana na wenzake Suleiman Lempaa na Sophia Rajab, walikuwa na wakati mgumu kushughulikia wateja wao kupelekwa mahakamani.

Kukamatwa kwa bloga huyo wa upinzani pia kunahusishwa na jumbe anazochapisha mitandaoni kupitia akaunti zake, akikosoa serikali ya Rais William Ruto hasa inavyoangazia maandamano ya Azimio.

  • Tags

You can share this post!

Alishwa kifungo cha miezi 36 jela kwa kutusi mkewe

Mtoto Sagini: Hukumu kwa waliomng’oa macho kutolewa...

T L