• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Wataalamu wapendekeza sheria za mifugo zitathminiwe kuipunguzia dhuluma

Wataalamu wapendekeza sheria za mifugo zitathminiwe kuipunguzia dhuluma

NA SAMMY WAWERU

KUNA haja sheria za mifugo nchini zitathminiwe ili kuipunguzia na kuindolea dhuluma zinazotekelezwa na binadamu.

Shirika la Mifugo Nchini (DVS) limesema uhayawani unaotendewa wanyama, utadhibitiwa kupitia mageuzi ya sheria zinazolinda mifugo.

Kauli hiyo imejiri wakati ambapo World Animal Protection, shirika la kimataifa lisilo la kiserikali na linalotetea maslahi ya wanyama kuibua malalamishi haki za mifugo nchini kukiuka.

Shirika hilo, mwaka uliopita, 2021, lilifanya utafiti katika vichinjio kadha nchini na kubaini mifugo hupitia ukatili.

Uchunguzi wa World Animal Protection pia ulishirikisha shughuli za ufugaji na usafirishaji mifugo kichinjioni.

“Inahuzunisha kuona wanavyosafirishwa kwa magari na pikipiki,” taarifa ya shirika hilo ikaelezea.

Liliibua malalamishi jinsi ambavyo mifugo hulishwa na kupewa maji, mfumo wa usafirishaji ukitiliwa shaka wanavyofungwa kwa kamba haswa wanapobebwa kwa kutumia pikipiki.

“Dhuluma kwa mifugo zitaangaziwa sheria zinazopaswa kuwalinda zikitathminiwa, na kuzindua zinazopendekeza hatua kali kuchukuliwa kwa wanaokiuka haki,” amesema Dkt Jane Njuguna, kutoka DVS.

Alitoa mapendekezo hayo akizungumza jijini Nairobi, katika hafla iliyoandaliwa na wadauhusika sekta ya mifugo.

Huku asilimia 80 ya ardhi ya Kenya ikiwa jangwa na nusujangwa, idadi kubwa ya wakazi wakiendeleza ufugaji, Dkt Jane alisema mifumo ya kilimo na ufugaji inapaswa kubadilishwa.

“Chakula cha mifugo kinapaswa kuwa salama, na kilichoafikia virutubisho faafu,” akasema afisa huyo.

World Animal Protection imekusanya saini za mswada unaopendekeza upigaji marufuku mfumo wa ufugaji wanyama wengi kwenye eneo moja, na kulishwa chakula chenye madini kuharakisha ukuaji (factory farming).

Baadhi ya vyakula hivyo, vimezalishwa kwa kutumia fatalaiza na dawa zenye kemikali na ni hatari kwa wanyama na binadamu (kupitia nyama).

Vizimbani au zizini, mifugo na ndege ni sharti kuwa huru kutembea, kucheza na kutangamana, mfumo maarufu kama deep litter system kwa Kiingereza.

Kwenye vichinjio, shirika hilo linapendekeza mifumo bora ya uchinjaji ikumbatiwe ili kupunguza dhuluma kwa mifugo.

Isitoshe, mifugo inapowasili inapaswa kulishwa chakula na kunyweshwa maji.

Aidha, World Animal Protection inasisitiza mifugo haipaswi kuwekwa vichinjioni zaidi ya saa 18.

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: Wataalamu sasa waonya kuwa kuumwa na kichwa...

‘Mawaziri wako huru kuunga Raila mkono’

T L