• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Zafarani na faida zake

Zafarani na faida zake

NA MARGARET MAINA

[email protected]

ZAFARANI – Saffron – ndicho kiungo cha bei ghali zaidi duniani.

Sababu ya bei yake kuwa ni ya juu ni njia yake ya uvunaji, ambao ni wa kazi nyingi hivyo kufanya uzalishaji wake kuwa wa gharama kubwa. Zafarani huvunwa kwa mkono.

Zafarani hukaushwa na kutumika kama kiungo kwa vyakula na pia kutia rangi kwa vyakula na bidhaa nyingine.

Zafarani husaidia kulinda seli zako

Zafarani ina misombo inayoweza kulinda seli zako dhidi ya mikazo ya oksidi. Zafarani ina ladha na harufu yake tofauti na nzuri inaweza kusaidia kuboresha hisia zako, kumbukumbu, na uwezo wa kujifunza, na pia kulinda seli za ubongo wako dhidi ya mkazo wa oksidi.

Misombo inayopatikana katika maua ya zafarani, ina manufaa ya kiafya kama vile kupunguza uvimbe, pamoja na kutumika kama dawa dhidi ya mfadhaiko.

Inaweza kuboresha hisia na kutibu dalili za mfadhaiko

Zafarani inaweza kusaidia kuangaza hisia zako. Virutubisho vya zafarani vinatibu dalili za unyogovu wa wastani.

Inaweza kupunguza hamu ya kula na kusaidia kupunguza uzani uliopitiliza

Mazoea ya kula vitafunio mara kwa mara yanasababisha mtu kuongeza uzani kupitiliza. Zafarani inaweza kuzuia hamu yako ya kula vitafunio mara kwa mara. Unapotumia virutubisho vya zafarani, utahisi kushiba zaidi, na utapoteza uzani zaidi. Nadharia moja ni kwamba zafarani huinua hali yako, ambayo inapunguza hamu yako ya kula.

Hupunguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa ya moyo

Antioxidants katika zafarani zinaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa. Zafarani ina potasiamu nyingi, kwa hivyo, ulaji wa mara kwa mara wa zafarani husaidia kupanua mishipa ya damu, hivyo hupunguza shinikizo la damu ili kuzuia ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Pia ina faida za kupunguza lehemu mbaya au hatari katika damu yako. Vile vile huzuia kuzibika kwa mishipa ya damu hivyo, inapunguza hatari yako ya mshtuko wa moyo au shida zinazohusiana na moyo. Zafarani pia huongeza au kuimarisha kinga yako.

  • Tags

You can share this post!

Waiguru amsihi Rais Ruto afufue ujenzi wa miradi ya maji

Gor yaangushia TUK mvua ya magoli kirafiki

T L