• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Gor yaangushia TUK mvua ya magoli kirafiki

Gor yaangushia TUK mvua ya magoli kirafiki

Mnamo Jumamosi K’Ogalo ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Bidco United katika uga wa Kaunti ndogo ya Thika. Mshambuliaji Peter Nzuki alifungia Bidco United lakini Gor ikasawazisha kupitia Dennis Ng’ang’a.

Katika mechi ya Jumapili iliyogaragazwa Camp Toyoyo, mtaani Jericho, washambuliaji Loyd Khavuchi na Enock Wanyama, walifunga mabao mawili kila moja huku Boniface Omondi, Sydney Ochieng’ na Parmenus Ochola, wote wakifunga goli kila mmoja.

Wenyeji walifunga kupitia penalti ya Peter Otieno.

K’Ogalo imekuwa ikitumia mechi hizi kujifua kwa msimu mpya ambao bado haufahamiki utaanza lini baada ya klabu kushikilia kuwa zitashiriki tu ligi inayotambulika na Sjirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Kenya iliangushiwa marufuku ya Fifa mnamo Februari baada ya utawala uliopita kupiga darubini usimamizi wa soka.

Kocha wa Gor Mahia Johnathan McKinstry alifurahia ushindi huo ila akasema bado anamakinikia kuhakikisha vijana aliowatoa kutoka kikosi chipukizi wanavyocheza.

“Hiki kikosi kinaendelea kuiva na nina imani watafanya vyema msimu ujao. Hatumakinikii sana ushindi bali jinsi tunavyocheza ili kutathmini maendeleo ya vijana hao chipukizi,” akasema raia huyo wa Ireland ya Kaskazini ambaye ana umri wa miaka 37.

Pia kocha wa Bidco United Anthony Akhulia alisema kikosi chake kitaendelea na mechi za kimarafiki ili kujinoa kwa msimu mpya.

“Vijana wangu wanajituma na nina baadhi ya wachezaji wapya kikosini ambao ninawafuatilia. Ni kupitia mechi hizi za kirafiki ambapo tutafuatilia jinsi walivyocheza. Tuna matumaini kuwa utata wa Fifa utasuluhishwa hivi karibuni,” akasema Akhulia.

  • Tags

You can share this post!

Zafarani na faida zake

Tiba za nyumbani za kukusaida endapo umechomwa na jua

T L