• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
WANDERI KAMAU: Tukome kumlaumu shetani kwa kutojali na mapuuza yetu ya kila siku!

WANDERI KAMAU: Tukome kumlaumu shetani kwa kutojali na mapuuza yetu ya kila siku!

NA WANDERI KAMAU

MIONGONI mwa jamii za Kiafrika, kumekuwa na simulizi nyingi kwamba wakati mtu anapofariki ama kujipata katika ajali fulani “huwa si matamanio yake kujipata katika hali hiyo”.

“Wajua ajali haina kinga. Wakati wake ulikuwa umefika….”

Ndizo baadhi ya simulizi ambazo huandama matukio hayo.

Hata hivyo, ukweli ni kuwa, baadhi ya ajali husababishwa na hali ya kutojali miongoni mwetu.

Hivyo, hatupaswi kumwelekeza Shetani lawama zote kutokana na kutojali kwetu.

Kwa mfano, mnamo Jumanne, kuna video moja iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikionyesha mwendeshaji bodaboda akitishia kuvuka katika mto mmoja uliojaa maji katika Kaunti ya Narok.

Kwenye video hiyo, baadhi ya watu wanasikika wakimwambia: “Vuka! vuka!”

Pengine kwa kuonekana kushawishika na rai za watu hao, mwanabodaboda huyo aliamua kuvuka mto huo bila kujali hatari iliyomkabili.

Baada ya sekunde chache, alisombwa na maji pamoja na pikipiki yake aliposhindwa kuhimili nguvu na kasi ya maji hayo.

Mnamo Jumatano, polisi katika kaunti hiyo walisema wamefanikiwa kuupata mwili wa mhudumu huyo pamoja na pikipiki yake.

Bila shaka, hiki si kisa cha kwanza kinachohusu kifo ama vifo vya watu waliosombwa na mito kwa kupuuza nguvu na kasi ya maji.

Hata hivyo, cha kushangaza ni kuwa, watu wengi huonekana kutojifunza kutokana na matukio hayo.

Bila shaka, kifo hiki kingezuiwa ikiwa tu mhudumu huyo angengoja maji hayo kupungua na kupuuza kauli za ‘mashabiki’ wake.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Kwaheri 2022, mwaka uliokuwa ‘mrefu...

TAHARIRI: Uamuzi wa seneti ni funzo kwa magavana, madiwani

T L