• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
FARHIYA HUSSEIN: Pengo waliloacha Ngala, Nassir na Maitha halijazibwa Pwani

FARHIYA HUSSEIN: Pengo waliloacha Ngala, Nassir na Maitha halijazibwa Pwani

NA FARHIYA HUSSEIN

H UKU ikiwa imesalia takriban miezi mitano kabla Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, mjadala kuhusu ni nani atarithi nafasi zilizoachwa na vigogo wa awali wa Pwani waliofariki Ronald Ngala, Karisa Maitha na Shariff Nassir umeanza.

Watatu hao walisifika kuwa mstari wa mbele kupigania na kutetea maslahi ya Wapwani.

Kwa muda mrefu, wengi wamekuwa wakimtaja Gavana wa Mombasa Hassan Joho kama anayetosha kuvalia viatu vyao.

Hii ni kutokana na namna alivyojikuza kisiasa tangu alip – owania ubunge Kisauni kwenye uchaguzi mdogo mnamo 2004.

Wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuwa na uwezo wa kuendeleza maslahi ya Wap – wani, ni Gavana wa Kwale, Bw Salim Mvurya na mwenzake wa Kilifi, Bw Amason Kingi.

Ronald Ngala alifahamika kwa kuipa kipau mbele na kupigania masuala ya Pwani kwa ukakamavu.

Safari ya kisiasa ya Ngala ilimletea sifa kimataifa wakati Waafrika walikuwa wakisimama kwa pamoja kutafuta uhuru

wao. Ngala aliwahi kuchaguliwa kuwa mweka hazina wa KANU, lakini baadaye akajiunga na KADU, na kuchaguliwa kiongozi wa chama hicho.

Hakutazama nyuma kwa misimamo yake ya kukomboa Wapwani na akawa mwanasiasa maarufu wa jamii ya Mijikenda na pia kutoka Mkoa wa Pwani katika miaka ya 1950 na 1960, hadi kifo chake mnamo 1972.

Kufuatia kifo chake, Nassir na Maitha walisifika kwa kufuata nyayo za Ngala, kwa namna walivyojaribu kutetea Wapwani katika serikali ya kitaifa.

Nassir alikuwa karani kabla ya kuwa Waziri wakati wa utawala wa Rais Daniel arap Moi.

Alisifika sana kwa juhudi zake za kutoogopa kuuza ajenda za chama cha KANU katika eneo hilo.

Alipewa jina la mfalme wa kisiasa kutoka eneo la Pwani kwa

vile alikuwa kiongozi mahiri wa kisiasa kuhusiana na mada za majimbo. Alikuwa waziri wa pili wa Kiislamu akiungana na Hussein Maalim Mohammed. Alifariki 2005.

Kwa upande wake, safari ya kisiasa ya Maitha ilianza kama diwani 1979 kabla ya kuwashinda Rashid Mzee na Said Hemed 1997 na kuibuka mshindi wa kiti cha Ubunge cha Kisauni.

Aliteuliwa katika Baraza la Mawaziri la Rais Mwai Kibaki akiongoza Utalii na Wan – yamapori.

Maitha alijulikana kwa kuwa shupavu na kutetea bila woga ajenda za Pwani zilizompa jina la ‘Mugogo’ alilopewa na watu wa asili yake jamii ya Mijikenda.

Swali ambalo linazidi kujitokeza ni je, nani atakayekaa meza kuu kujadili kwa niaba ya wenyeji wa Pwani? Nani atachukua nafasi ya vigogo wale watatu waliotuacha?

  • Tags

You can share this post!

Chama chaomba korti iruhusu uhamaji wa wawaniaji

Kang’ata asema chama cha Jubilee ni meli iliyozama

T L