• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
JUMA NAMLOLA: CBC: Waingereza husema huwezi kuila keki yako na utarajie kuwa nayo

JUMA NAMLOLA: CBC: Waingereza husema huwezi kuila keki yako na utarajie kuwa nayo

NA JUMA NAMLOLA

UNAPOMTAJA Walter Elias, hakuna anayefahamu unayemzungumzia, bila kuongeza jina Disney. Mwamerika huyo aliyekuwa na asili ya Uingereza, anatambuliwa ulimwengu mzima kwa katuni yake maarufu ya Mickey Mouse.

Ingawa alikufa miaka 56 iliyopita, Walt Disney anaendelea kufurahisha watu kwa vibonzo vyake. Kwenye mojawapo ya nukuu zake nyingi, Disney aliwahi kusema, “Ndoto zetu zote zinaweza kutimia, ikiwa tutakuwa na ujasiri wa kuzifuatilia.”

Serikali tangu ilete mageuzi ya mfumo wa elimu kwa kuondoa ule wa 8-4-4 na kuleta CBC, kumekuwa na juhudi za kuonyesha mfumo huo hauna kasoro. Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amekuwa akizunguka kila pembe ya nchi akiwakemea wazazi kwamba hawajui wasemacho.

Tangu jana, wanafunzi wa Gredi za Tatu, Nne na Tano wamekuwa na mtihani. Kwa wale wa Grezi za Nne na Tano, alama zitakazopatikana baada ya mtihani huo, zitawekwa kwenye hifadhi ya mtandao wa Baraza la Mitihani (KNEC) pamoja na wizara ya Elimu.

Alama hizo zitatumika baadaye kuamua kama wanafunzi hao wana ujuzi au umilisi katika masomo wanayofanya.

Ingawa serikali iliagiza mtihani huo ufanywe ndani ya darasa na kusahihishwa na mwalimu anayewafunza watoto, haijaeleza ni vipi itatumia alama hizo kuamua hatima ya wanafunzi. Katika karne hii ambapo walimu hufuatiliwa utendakazi wao na mwajiri wao (TSC), hakuna mwalimu atakayekuwa tayari kuwafelisha wanafunzi. Tumekuwa tukiona jinsi walimu wamekuwa wakiiba wanafunzi wao mitihani ya KCSE ili shule zao zionekane zinafanya vyema kimasomo.

Kuwaachia walimu wa madarasa ya Gredi za Nne na Tano kusahihisha mitihani wenyewe, ni kuruhusu kuvurugwa takwimu za uhalisia wa mfumo wa CBC. Serikali inaweza kuamua kuwa mwanafunzi ni bora katika somo ambalo hana umilisi nalo.

Inachofanya serikali ni kuwatumia wanafunzi kama vifaa vya majaribio ya mfumo wa elimu ambao haujathibitishwa kuwa bora kuliko mifumo mingine.

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau matatizo yalianza...

CHARLES WASONGA: Zipo sheria za kutosha kukabili biashara...

T L