• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau matatizo yalianza serikali ilipoondoa mpango wa awali wa kutoa mbolea kwa bei nafuu kwa wakulima

TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau matatizo yalianza serikali ilipoondoa mpango wa awali wa kutoa mbolea kwa bei nafuu kwa wakulima

WAZIRI wa Kilimo Peter Munya ametangaza kuwa wizara yake imeandaa taarifa kuhusu mikakati ya kupunguza bei ya mbolea kabla ya kuanza kwa msimu wa upanzi.

Hii ni kufuatia malalamishi kutokwa wakulima wa mahindi kwamba bei ya bidhaa hiyo imepanda hadi Sh6,000 kwa gunia moja la kilo 50 katika maduka ya rejareja. Wengi wao sasa wanaonya kuwa ikiwa bei hiyo haitapunguzwa hawatapanda zao hilo mwaka huu.

Lakini Bw Munya asije akasahau kuwa bei ya pembejeo hii ya kilimo ilianza kupanda mnamo 2019, pale wizara yake kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha zilipoondoa mpango wa awali wa kutoa mbolea kwa bei nafuu kwa wakulima.

Serikali hii hii anayoihudumia ndio iliahidi, mnamo 2014, kujenga kiwanda cha mbolea nchini.

  • Tags

You can share this post!

Afisa ahimiza vyombo vya habari viwe vikimulikwa ili...

JUMA NAMLOLA: CBC: Waingereza husema huwezi kuila keki yako...

T L